“Watching my family die to these philly streets,” ......“Probation is the only thing that got me tied to come coming back here so frequent!! My mission is to save my family from these streets and change the mindframe of all my lil cousins growing up in it!!!! #RIPLO hurt me to see you in this same spot lifeless!”.Aliandika Meek Mill.
Maafisa wa Polisi wa South Philadelphia wanadai kuwa Angelo na rafiki yake wakiwa nnje ya moja ya migahawa kwenye mitaa ya mji huo majira ya saa nne usiku,walishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu waliokua ndani ya gari ambapo Angelo alifariki kutokana na jeraha kubwa la risasi alilopata kichwani huku rafiki yake akijeruhiwa vibaya mguuni na risasi.
Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha mauaji ya Angelo ambaye nae alikua rapper,akifahamika kama LO,ambapo mapema mwaka huu aliachia video ya wimbo wake mpya unaofahamika kama Got That Bang.
Mnamo mwezi July mwaka huu,Meek Mill alitangaza kuwa mara baada ya kutoka kwa Mixtape yake ya "D4C",ataacha kuimba nyimbo zinazohamasisha fujo na matumizi ya silaha,kama sehemu ya mpango wa kupunguza matukio ya kihalifu kwenye jamii,hasa matumzi ya silaha za moto.
“AFTER DC4 I won’t continue to rap about extreme violence,” .......“But I will remain to let my people know in these terrible environments to adapt and survive at any cost because US BLACK PEOPLE ARE STILL AT WAR WITH OURSELVES AND THE SYSTEM IN REAL LIFE.” .Aliandika Meek Mill.