Thursday, September 15, 2016
Birdman adai kuwa Lil Wayne atakula jeuri yake.
Jino Kwa Jino..!! Hivyo ndo tunavyoweza kusema kwani siku kadhaa tu baada ya rapper Lil Wayne kudai kuwa hatakaa afanye tena kazi na rapper Birdman ambae hapo awali alikua Boss wake chini ya lebo ya YMCMB,Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa maswahiba hao wa zamani zinadai kuwa ugomvi wao unaweza kuwa mkubwa kuliko unavyofikiriwa.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ,watu wa karibu kutoka kwenye kambi ya Birdman wanadai kuwa kitendo cha Wayne kuendelea kuzungumzia ugomvi wake na Birdman kunaongeza chuki kati ya wawili hao kwani kutokana na Wayne kutangaza kuwa hatafanya tena kazi na Birdman,Hatimae Boss huyo wa Cash Money amepigilia msumari uamuzi wake wa kutotoka kwa album ya Wayne inayofahamika kama "Tha Carter V's" ambayo ilisharekodiwa.
"Tha Carter IV",ndiyo album ya mwisho ya Wayne kutoka akiwa chini ya Cash Money.
Hata hivyo huenda album hiyo ya Wayne "Tha Carter V's" inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake ikabaki kuwa simulizi ya kusadikika kwani kutoka kwa album hiyo kunategemea uamuzi wa kisheria juu ya madai ya Wayne anaetaka kulipwa $51m na Cash money,$10 kama malipo ya awali ya album yake ya "Tha Carter V's" sambamba na kiasi kingine cha malipo ya mirahaba ya wasanii walio chini ya lebo yake ya Young Money iliyokua sehemu ya YMCMB.
Mgogoro kati ya wawili hawa ulipelekea Wayne kupost ujumbe uliozua utata kwenye mitandao ya kijamii,ujumbe uliotafsiriwa kuwa huenda rapper huyo yupo mbioni kuachana na muziki,Tetesi ambazo amezikanusha.
“If that [tweet] was at 3:30 [a.m.], I probably was at the studio at 6,” .......“Undisputed.”.... “The height of my talent or the height of my career, I haven’t reached that at all.”.Alisema Wayne kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha FOX.
Comments System
facebook