Showing posts with label Udaku. Show all posts
Showing posts with label Udaku. Show all posts

Wednesday, December 14, 2016

Video : Amber Lulu Alipokutana Na Mtoto Wa Young Dee

 Wikiendi iliyopita a rapa Young Dee alithibitisha kumkubali mtoto wake aliyemkataa kabla ya kuzaliwa kwake. Mastaa mbalimbali walijitokeza kumpongeza kwa maamuzim hayo. 
 
 Anajulikana kama Amber Lulu moja kati ya warembo hotcake kwenye videos za wasanii mbalimbali wa Bongoflava ambae amekua akitajwa kutoka kimapenzi na Young Dee hakubaki nyuma kwani alizidi kuonesha mapenzi yake ya dhati kwa rapa huyo baada ya kuonekana kwenye pozi tofauti na mama mtoto wa Young Dee pamoja na Mtoto Tammy.


JIONEE HAPA ILIVYOKUA:


Friday, November 11, 2016

Hizi Hapa Salaam Za Shilole Kwa Nuh Mziwanda Saa Chache Baada Ya Kufunga Ndoa.

Jana Novemba 10 mwanamuziki Nuh Mziwanda aliuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake Nawal maarufu Mrs. Mziwanda.
 Mastaa mbalimbali wamempongeza Nuh Mziwanda kwa hatua hiyo, Moja kati ya watu ambao wamejitokeza kumpongeza Nuh ni Mama la Mama Shishi Beybe Himself, ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram amewapost maharusi hao na kuwasindikiza na ujumbe wa pongezi.
 "Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie Baraka tele kwenye ndoa yenu" Ameandika Shilole..

Ikumbukwe Shilole na Nuh Mziwanda wamewahi kuwa wapenzi wa muda mrefu ambao baadae waliachana na kila mtu kufanya yake.
 Kitendo cha Shilole kuwapongeza wanandoa hawa ni dhahiri wazi hakuna beef kati ya zilipendwa hao kama ambavyo Shilawadu na wadau wengine tunavyofikiria...

Thursday, October 27, 2016

Birthday Ya Aunty Ezekiel Yamshawishi Lulu, Aahidi Kuzaa Kesho

Kutoka kwenye kiwanda cha filamu za Kitanzania leo Oktoba 27 muigizaji Aunty Ezekiel anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
 Kama ilivyo kawaida ya matumizi ya mitandao ya kijamii kila linapokuwepo tukio maalum wahusika na watu wao wa karibu hutumia mitandao hiyo kufikishiana ujumbe zikiwemo pongezi na salaam mbalimbali,
Aunty Ezekiel ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa kupost picha tofauti zikimuonyesha yeye na famil;ia yake yaani Baba mtoto wake Mose Iyobo na mtoto wa Cookie..


Elizabeth Michael "Lulu" ambae pia ni muigizaji wa Bongo muvi alishindwa kuvumilia kabisa kutokana na picha ambazo Aunty Ezekiel amezipost na kujikuta akitokwa na maneno haya ambayo wazi wazi yameonekana ni utani kwa Aunty na mtoto wake (Cookie)

"Nazaa Kesho....Nimepanic😫😫😫😫😫 @auntyezekiel najitolea kununulia album dada insta sio mahala sahihi kwa hivi vipicha vyako...tupo wanafunzi humu😭wengine bado under 18 ila naona unatushawishi😭hujui serikali inapiga vita mimba Za utotoni we dada😫Sitopenda kushawishika kwa hv vi picha vyenu 😫😫😭Cookie Ana 🐸 pia Shabaaaaaash....nadhani nimeshikwa na uchungu maana naandika caption huku nahangaika🙄😵Kesho jmn naenda kujifungua 😬😬😬😬
Sijui kama Leo ni bday yako naona kukomoa day tu😭😭😭" Ameandika Lulu..

Saturday, October 1, 2016

Esma Amkana Diamond Mbele Ya Wanahabari


Wote tunawajua Queen Darlin na Esma Khan kama madada wa mbongoflava Diamond Platnumz,
 Unafahamu mahusiano yao vizuri?,
 Diamond Platnumz anashare Baba na Queen Darlin hukun upande wa mama akiwa anaungana na Esma Khan.
 Hivi juzikati Esma Khan alipata alipata  nafasi ya kuongea na waandishi wa habari, Sikia alichokisema kuhusu undugu wao.



Sasa Dada yetu huo uarabu na uswahili umetoka wapi tena?, Haya Hupendi wakujue kama wewe ni Dada yake Mondi sasa mbona kwenye instagram inaonekana Baba yenu mmoja.

Cheki Matusi Ya Davido Kwa Mashabiki Wake.


Mwanamuziki Davido ameamua kusambaza upendo kwa mamia ya mashabiki wake aliokutana nao ndani ya supermarket ya Shoprite kwenye moja kati ya mall za jijini lagos nigeria.

Mkali huyo wa hit song kama Skelewu, Fans Mi na The Sound amefanya kile kilichotafsriwa “Suprise” baada ya kuwanunulia Ice Cream mashabiki wote waliokuwepo maeneo hayo.


ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI:


Friday, September 23, 2016

VIDEO:Mzazi mwenza wa Ben Paul atoa ya moyoni baada ya Ben Paul "Kudendeka" na Snura.



Wiki chache baada ya picha kusambaa mitandaoni zikimuonesha Hit Maker wa ngoma kali za R&B,Ben Paul akidendeka na Mwanamuziki Snura Mushi walipokua Mkoani Singida kwenye Tamasha la Fiesta,ambapo pia walioekana mara kadhaa wakikumbatiana na kupigana mabusu wakiwa kwenye moja ya majukwa ya Fiesta,Hatimae mzazi mwenza wa Ben Paul,Latifa Mohamed,amedai kuwa kamwe hawezi kumfatilia mtu kwani aliagwa na Ben kuwa anaenda kazini,hivyo anachojua Ben Paul yupo kazini.


             Snura.

Tazama Mahojiano yake na Clouds E.







French Montana amvisha Iggy Azalea pete saba za "Diamond".


MAHABA NIUE..!! Hivyo ndo tunavyoweza kusema kwani kwa rapper French Montana anaonekana kuzama kwenye penzi na rapper Iggy Azalea baada ya Iggy kupost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha kiganja chake kilichovishwa pete saba za almasi huku akiambatanisha na ujumbe unaosomeka...“He told me pressure makes diamonds,”.Ameanika Iggy Azalea ambae hapo awali alikua kweye mahusiano na mcheza kikapu wa ligi kuu ya Marekani (NBA),Nick Young.
A photo posted by Iggy Azalea (@thenewclassic) on


Hii si mara ya kwanza kwa wawili hawa kuweka wazi mapenzi yao kwani mwezi uliopita zilisambaa picha zikiwaonesha waki-kiss walipokua mapumzikoni nchini Mexico.





Thursday, September 22, 2016

VIDEO:Diamond amrudisha Wema Sepetu kwa Idris Sultan kiaina.



Wakati kasheshe la kukutwa kwa hereni ya Mwanamke chumbani kwa Mama watoto wake Zari The Boss Lady likiendelea kufukuta,Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond amepost video ya aliekua X-Girl wake Madam Wema Sepetu akiimba wimbo wake mpya "Salome" na kuandika ujumbe ambao baadhi ya mashabiki wanahisi Diamond anajaribu kulirudisha penzi kati ya Mshindi wa BBA-2015 Idirs Sultan na Wema Sepetu ambao mapenzi yao yanadaiwa kuyeyuka tangu mwanzoni mwa mwezi July Mwaka huu.


"Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini....??? Tisha sana #SALOME wake @idrissultan full Video link in my BIO and @rayvanny BIO☝.....Shukran sana".Ameandika Diamond.


 Hizi ni baadhi ya coment za mashabiki;
 

PICHA:Mwenye hereni iliyokutwa chumbani kwa Diamond abainika.

 Mama watoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz,Zari The Boss Lady ameendele kutupa madongo kwa wanawake anaohisi wanatoka kimapenzi na Diamond baada ya kupost video kupitia mtandao wa "Snapchart" akiandika ujumbe kwenda kwa mwanamke anaedai ameacha hereni kwenye moja ya vyumba vyake bila kumtaja jina.

 Kupitia mitandao ya kijamii kumwekua na picha inayosambaa ikionesha picha ya hereni inayodaiwa kukutwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba ya Diamond,Madale Tegeta huku upande wa pili ikionekana sura ya Mwanamitindo Hamisa Mabeto ambae hereni aliyovaa katika picha hiyo inafanana na hereni iliyozua kasheshe.






  Posts hizo za Zari zinaendelea kukuza tetesi za muda mrefu juu ya  usaliti kwenye  mahusiano yake w na Diamond hivyo pengine Mwanamama huyu ambae ana ujauzito wa pili kwa Hit maker wa singo ya "Kidogo",ameamua kuchukulia poa kuivumilia tabia ya Diamond japo suala hili linaweza kuchafua hali hewa kwenye mahusiano ya mastaa hawa.
Ikumbukwe kuwa kwa muda sasa Mwanamitindo Hamisa Mabeto amekua akiandamwa na skendo ya ku-share kitanda na Diamond ambae amekua akikanusha madai hayo,ambapo hata hivyo Mwanamuziki huyo amekuza tetesi hizo mara baada ya Hamisa kuonekena kama "Video Queen" kwenye video ya wimbo mpya wa Diamond aliomshirikisha Ray Vany unaofahamika kama "Salome"




Kwa post hii ni kweli kuwa Mwana FA ana bifu na GK..?

Kundi la East Cost lililokua likiundwa na rappers wakali kama King Crazy-GK,AY,Mwana FA,Buff G,Snare na wengine wengi lilitikisa anga ya muziki kati ya mwaka 2003 hadi 2007  kabla kundi hilo kumeguka vipande vipande ambapo AY na Mwana Fa walijitoa na kuuanza ku-release kazi zao nnje ya  kundi hilo ambalo lilibaki mikononi mwa GK.

                                               Mwana FA.

Ni muongo mmoja sasa tangu East Cost imeguke ila mapema mwezi huu rapper King Crazy-GK amerudi kwenye game ya muziki kwa kuachia wimbo na video mpya ya wimbo wake unaofahamika kama "Mzuri Pesa".


Kupitia akaunti yake ya Facebook,Mwana Fa amemtania GK kutokana na aina mpya ya muziki alioamua kufanya kwa kupost "Cover" ya wimbo huo na kuandika   ..."Ngoja ngoja..masihara kando na ni kwa sababu zifuatazo;..hardcore lina instagram account ambayo ni @kingcrazy_gk makofi tafadhali..lina wimbo wa kuimba narudia haljarapa limeimba hilo hardcore...makofi tena jamani....hardcore hili lina video kali sana kwenye bio yake kuna link ama you tube...ngoma inaitwa MZURI PESA...nasema hiviii ni hayo tu kwa leo..ahsanteni".Ameandika FA.


PICHA:Anaetajwa kuvunja ndoa ya Brand Pitt na Angelina Jolie huyu hapa.

BRANGELINA SAGA...!!  Wakati penzi la waigizaji nguli kwenye soko la filamu ulimwenguni likifika tamati  baada ya Angelina Jolie (41) kudai talaka kutoka kwa mumewe Brand Pitt (52),Hatimae chanzo cha  talaka kimebainika baada watu wa karibu wa wanandoa hao wa zamani kuadai kuwa Jolie alimwajiri paparazi ambae alikua akifatilia nyendo za mumewe ambapo taarifa zinadai kuwa Brand Pitt anadaiwa kumsaliti mkewe na  mwigizaji raia wa Ufaransa Marion Cotilard (40).

     Brand Pitt na Marion Cotilard wakati wakirekodi vipande vya filamu ya "Allied".

                Marion Cotllard.

Taarifa ya Paparazi huyo imebainisha kuwa Pitt alikua akichepuka na Cotillard wakati waki-shoot filamu mpya inayofahamika kama "Allied" ambapo wawili hao wanadaiwa ku-share kitanda pamoja wakiwa kambini huku Pitt akiwahadaa watu kuwa yupo peke yake kwenye hoteli aliyofikia wakati upigaji wa picha wa filamu hiyo Jijini London.

     Brand Pitt na Angelina Jolie.

 Kwa upande wake Cotilard amepuuzia madai ya kutoka kimapenzi na Pitt na kudai kuwa bado yupo kweye mahusiano na ana ujauzito wa pili kwa mpenzi wake wa siku nyingi raia wa Ufaransa ambae ni Director wa filamu anaefahamika kama Guilaume Canet ambae licha ya kuwa nae kwenye mahusiano tangu mwaka 2007 na kufanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja,hawajafunga ndoa.


Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa TMZ,baadhi ya marafiki wa wanandoa hao  wanadai kuwa tabia ya Brand Pitt ya unywaji Pombe na uvutaji Sigara uliopitiliza inaweza kuwa chanzo cha Jolie kudai talaka kwani Pitt amekua mbali na masuala yanayoihusu familia yake kutokana aina mpya ya maisha aliyochagua.
 Brand Pitt na Angelina Jolie wamekua kwenye mahusiano tangu mwaka 2004,ambapo mwaka 2014 walifunga ndoa.Mahakama imetangaza tarehe 15,Sept.2016 kama siku ambayo wawili hao walitengana rasmi ambapo katika shauri hilo la madai,Jolie aliwakilishwa mahakamni na wakili wake Laura Wasser akitaka haki ya malezi ya watoto wao sita wakiwemo walioasiliwa na familia yao - Maddox,Pax,Zahara,Shiloh na mapacha Knox na Vivienne aliozaa na Pitt.


Baadhi ya filamu maarufu zilizochezwa na wanandoa hawa waliotegana ni pamoja na "Mrs & Mr.Smith" (2005) pamoja na "By the Sea" iliyotoka mwaka 2015.


Unaikumbuka "Mrs. & Mr Smith",



Wednesday, September 21, 2016

VIDEO:Utacheka na majibu ya The Game kuhusu bifu yake na Meek Mill na ku-date na Kim Kardashian.

Rapper The Game ameeendeleza ubabe na kauli zenye utata kwani wakati ambao bifu yake na rapper Meek Mill ikizidi kutokota,huku chanzo cha bifu yao kikidaiwa kuwa ni madai ya The Game anaedai kuwa Meek Mill alipeleka taarifa za kizushi kwenye kambi ya Mwanamuziki raia wa Jamaica Sean Kingstone kuwa yeye na timu yake walihusika kwenye wizi wa cheni ya Sean Kingstone yenye thamani ya kisai cha  $300k.

Sasa basi kupitia kipindi cha "The Wendy Williams Show" The Game amefunguka baadhi ya mambo tusiyoyajua kuhusu bifu yake na Meek Mill,ishu ya yeye kutoka kimapenzi na baadhi ya warembo kutoka kwenye familia ya Kardashian girls,bifu yake ya zamani na 50 Cent bila kusahau ujuo wa album yake mpya aliyoipa jina 1992

Kuhusu Meek Mill: “It’s just a little hip-hop beef…We haven’t had a fight yet. It’s not a fight. It’s just hip-hop…It comes down to a point where, you’ve gotta deal with it as it comes. I feel like I was violated.”

 "Hii ni bifu ya kimuziki,ni shemu ya muziki wa Hip Hop,hatujafikia hatua ya kupigana...ila inaweza kumalizika nikiamua,Nadhani nimekosewa heshima"



Kuhusu maisha ya muziki na bifu : “Nobody’s perfect. We all have days where we’re at fault and we make mistakes. Some days are good. Some days are bad. You’ve got to take them all together.”

"Hakuna mtu aliekamilika,kuna muda huwa tunapotea na kufanya makosa,kuna wakati mzuri na wakati wa matatizo kwenye maisha.unatakiwa kukubaliana na kila hali"
 
 Kuhusu bifu yake na  50 Cent: “We were in a strip club in L.A. and I just stepped to him. We talked for about 15 minutes and we kind of hashed it out. We left on good terms…It’s over now.”

"Tulikutana Casino L.A,nilimsimamisha na tuliongea kama dakika 15,tupo vizuri...nadhani mimi na yeye tumemaliza"

Kuhusu Tamthilia ya 50 Cent ,“Power”: “I watch ‘Power.’ I definitely would [act in the series]. I like ‘Power.’ It’s a good show.”

"Huwa naitazama,natamani ningekuwemo ndani...ni show kali"


Kuhusu album yake mpya "1992": “1992 was the first year that I joined a gang. At that point in my life, I was getting pulled in both directions. I grew up in a Crip neighborhood but my brothers were Bloods. It was sort of a tug-of-war. That’s how it is in Compton. Once you get close to your teenage years, gangs start pulling at you. It’s almost 99 percent that you’ll probably join a gang.”

"Mwaka 1992 ndio mwaka nilioamua kuingia mtaani,Ni sehemu ya maisha ambapo nilikumbana na changamoto nyingi.Nilikulia kwenye mtaa ambao nilishuhudia ndugu zangu wakipoteza maisha,naweza kusema ilikua ni vita.Hayo ndo maisha ya mji wa Camton kwani baada ya balehe unajikuta ukivutwa kijiingiza kwenye makundi ya mitaani.Naweza kusema asiilimia 99 utakua sehemu ya makundi hayo"

Kuhusu kutoka kimapenzi na warembo wa familia ya Kardashians: “It was three [Kardashians]. It gets a little tricky. [Black] Chyna ain’t married yet…But it’s all good if it’s facts. And she cool too.”

"Yeah nimepita na watatu kati yao,ilinichanganya kidogo,....hata Blac Chyna pia...najua hajaolewa bado,ila ukweli unabaki kuwa tupo poa"
  
Kuhusu ku-sex na Kim Kardashian: “I’ll tell you this. Kanye is a really good friend of mine and they’ve got really beautiful kids and I don’t want to disrespect their family.”

"Nachoweza kusema ni kwamba Kanye West ni miongoni mwa marafiki zangu wakubwa,Mimi na yeye tuna watoto wazuri na sitaki kuikosea heshima familia yake"


Kuhusu ku-sex na  Khloe Kardashian: “Sometimes it gets late at night and people…I don’t know.”

"Muda mwingine najichanganya hadi usiku wa manane na watu...Sikumbuki"


Kuhusu ku-sex na Kourtney Kardashian: “No.”

"Hapana"

Kuhusu ku-sex na Kylie and Kendall Jenner: “They’re not Kardashians.”

"Hao sio sehemu ya hiyo familia"

PICHA:Profesa Jay na ndudu zake walivyosheherekea miaka 80 ya kuzaliwa kwa Baba yao.










Sunday, September 18, 2016

Tangazo kwa wanawake ambao hupiga kelele wakiwa "Guest".

Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaotembelea nyumba za kulala wageni maarufu kama "Guest House",hii inakuhusu.

Usishangae ukikutana na tangazo hili kwenye mlango wa chumba ulicholipia..!! 
 


Picha:Msichana aliejichora tatoo ya Ali Kiba baada ya kupagawishwa kitandani.

Wakati Ali kiba na Diamond walipokutana kwenye jukwaa moja mjini Mombasa kuna mambo mengi yaliyotokea nyuma ya pazia.Miongoni mwa issue zilizo-trend baada ya show kumalizika ni pale ambapo mrembo mmoja anaefahamika kama Bridget Achieng  alipoamua kuvujisha siri nzito kati yake na Ali kiba baada ya kuamua kuchora mchoro wa tatoo wenye jina la hit maker wa singo ya "Aje",Ali Kiba.
 Tetesi  zinadai kuwa,mrembo huyo alifikia uamuzi wa kuchora tattoo hiyo ya "King Kiba" baada kupagawishwa na shughuli ya Kiba kitandani kiasi cha kuamua kuchora tattoo hiyo kama  sehemu ya kukubali mtiti wa sita kwa sita kutoka kwa Mwanamuziki huyo.

A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him
Mrembo huyo amedai kuwa alijisikia mtu mwenye bahati kwa kuwa msichana pekee aliepata nafasi ya kumliwaza msanii huyo wakati alipokua mjini Mombasa na kuongeza kuwa tatoo hiyo itabaku kama kumbukumbu kwenye maisha yake kuwa aliwahi ku-kwichi-kwichi na King Kiba.
 A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him


A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him

Image result for ali kiba




Thursday, September 15, 2016

Birdman adai kuwa Lil Wayne atakula jeuri yake.


Jino Kwa Jino..!! Hivyo ndo tunavyoweza kusema kwani siku kadhaa tu baada ya rapper Lil Wayne kudai kuwa hatakaa afanye tena kazi na rapper Birdman ambae  hapo awali alikua Boss wake chini ya lebo ya YMCMB,Taarifa  kutoka kwa watu wa karibu wa maswahiba hao wa zamani zinadai kuwa ugomvi wao unaweza kuwa mkubwa kuliko unavyofikiriwa.

 Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ,watu wa karibu kutoka kwenye kambi ya Birdman wanadai kuwa kitendo cha Wayne kuendelea kuzungumzia ugomvi wake na Birdman kunaongeza chuki kati ya wawili  hao kwani kutokana na Wayne kutangaza kuwa hatafanya tena kazi na Birdman,Hatimae Boss huyo wa Cash Money amepigilia msumari uamuzi wake wa kutotoka kwa album ya Wayne inayofahamika kama "Tha Carter V's" ambayo ilisharekodiwa.
 "Tha Carter IV",ndiyo album ya mwisho ya Wayne kutoka akiwa chini ya Cash Money.

Hata hivyo huenda album hiyo  ya Wayne "Tha Carter V's" inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake ikabaki kuwa simulizi ya kusadikika kwani kutoka kwa album hiyo kunategemea uamuzi wa kisheria juu ya madai ya Wayne anaetaka kulipwa $51m na Cash money,$10 kama malipo ya awali ya album yake ya "Tha Carter V's" sambamba na kiasi kingine cha malipo ya mirahaba ya wasanii walio chini ya lebo yake ya Young Money iliyokua sehemu  ya YMCMB.

Mgogoro kati ya wawili hawa ulipelekea Wayne kupost ujumbe uliozua utata kwenye mitandao ya kijamii,ujumbe uliotafsiriwa kuwa huenda rapper huyo yupo mbioni kuachana na muziki,Tetesi ambazo amezikanusha.

“If that [tweet] was at 3:30 [a.m.], I probably was at the studio at 6,” .......“Undisputed.”.... “The height of my talent or the height of my career, I haven’t reached that at all.”.Alisema Wayne kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha FOX.



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.