Makada wa chama hicho walifunga ofisi hizo mapema leo alfajiri wakisema kuwa mwenyekiti huyo, Lengai Ole Sabaya hana hadhi tena ya kuwa mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha baada ya kughushi nyaraka za Idara ya Usalama wa Taifa kufanya utapeli.
Lengai Ole Sabaya,M/Kiti UVCCM-Arusha.
Baadhi ya makada ambao ni watiifu kwa Mwenyekiti huyo wameonekana wakimsaidia aweze kuingia ofisini wakijitahidi kuwaondoa waliokuwa wakimzuia bila mafanikio.
Baadhi ya picha wakati wa vurumai hizo;