Thursday, September 22, 2016

Chris Brown azuiwa kingia Japan,Mavazi yake mapya yatajwa kuwa chanzo.


Breezy alitarajiwa ku-perfom jijini Tokyo wiki ijayo ila taarifa zinadai kuwa maafisa usalama nchini Japan wamepiga marufuku kwa kwa Mwanamuziki huyo kutia maguu kwenye ardhi ya Japan kutokana sera za Taifa hilo kuwazuia watu wenye historia ya makosa ya udhalilishaji.


Hii si mara ya kwanza kwa Brown kukutwa na kadhia ya aina hii kwani amekua akiandamwa na vyombo vya uasalama  tangu mwaka 2009  alipompiga aliekua X-Girl wake na Mwanamuziki Rihanna.Chris Brown anaweza kukata rufaa lakini wanasheria wake wanahisi kesi hiyo inaweza kuwapotezea muda.


 Hata hivyo Mwanamuziki huyo amezindua logo mpya ya mavazi yake yanayofahamika kama "Black  Pyramid" ambapo amekua akiuza T-shirt zenye maandishi yanayosomeka "This B!tch Lyin" yakiambatana na picha ya Mwanamke anaefahamika kama Baylee Curran,ambae mapema mwezi huu alidai Chris Brown alimtishia na silaha nzito.

             Baylee Curran.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.