IRINGA:Mkfunzi mmoja katika Chuo Kikuu cha Mkwawa (MUCE) (Jina limehifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumtukana Rais Dkt.John Pombe Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.
Akizungumza na waandishi wa habari,Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Julius Mjengi alisema kuwa Mkufunzi huy (48) ameeleza kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo septemba 15 baada ya kutuma ujumbe wa maandishi unaomkashifu rais magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya jumanne,september 21 mkoani Rukwa ambapo alisafirishwa siku hiyo hiyo hadi Mkoani Iringa na kusomewa mashtaka yanayomkabili.