Thursday, September 22, 2016

PICHA:Anaetajwa kuvunja ndoa ya Brand Pitt na Angelina Jolie huyu hapa.

BRANGELINA SAGA...!!  Wakati penzi la waigizaji nguli kwenye soko la filamu ulimwenguni likifika tamati  baada ya Angelina Jolie (41) kudai talaka kutoka kwa mumewe Brand Pitt (52),Hatimae chanzo cha  talaka kimebainika baada watu wa karibu wa wanandoa hao wa zamani kuadai kuwa Jolie alimwajiri paparazi ambae alikua akifatilia nyendo za mumewe ambapo taarifa zinadai kuwa Brand Pitt anadaiwa kumsaliti mkewe na  mwigizaji raia wa Ufaransa Marion Cotilard (40).

     Brand Pitt na Marion Cotilard wakati wakirekodi vipande vya filamu ya "Allied".

                Marion Cotllard.

Taarifa ya Paparazi huyo imebainisha kuwa Pitt alikua akichepuka na Cotillard wakati waki-shoot filamu mpya inayofahamika kama "Allied" ambapo wawili hao wanadaiwa ku-share kitanda pamoja wakiwa kambini huku Pitt akiwahadaa watu kuwa yupo peke yake kwenye hoteli aliyofikia wakati upigaji wa picha wa filamu hiyo Jijini London.

     Brand Pitt na Angelina Jolie.

 Kwa upande wake Cotilard amepuuzia madai ya kutoka kimapenzi na Pitt na kudai kuwa bado yupo kweye mahusiano na ana ujauzito wa pili kwa mpenzi wake wa siku nyingi raia wa Ufaransa ambae ni Director wa filamu anaefahamika kama Guilaume Canet ambae licha ya kuwa nae kwenye mahusiano tangu mwaka 2007 na kufanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja,hawajafunga ndoa.


Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa TMZ,baadhi ya marafiki wa wanandoa hao  wanadai kuwa tabia ya Brand Pitt ya unywaji Pombe na uvutaji Sigara uliopitiliza inaweza kuwa chanzo cha Jolie kudai talaka kwani Pitt amekua mbali na masuala yanayoihusu familia yake kutokana aina mpya ya maisha aliyochagua.
 Brand Pitt na Angelina Jolie wamekua kwenye mahusiano tangu mwaka 2004,ambapo mwaka 2014 walifunga ndoa.Mahakama imetangaza tarehe 15,Sept.2016 kama siku ambayo wawili hao walitengana rasmi ambapo katika shauri hilo la madai,Jolie aliwakilishwa mahakamni na wakili wake Laura Wasser akitaka haki ya malezi ya watoto wao sita wakiwemo walioasiliwa na familia yao - Maddox,Pax,Zahara,Shiloh na mapacha Knox na Vivienne aliozaa na Pitt.


Baadhi ya filamu maarufu zilizochezwa na wanandoa hawa waliotegana ni pamoja na "Mrs & Mr.Smith" (2005) pamoja na "By the Sea" iliyotoka mwaka 2015.


Unaikumbuka "Mrs. & Mr Smith",



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.