Shekh Mkuu wa Tanzania Abubakari Zubeiry ametangaza jumatatu ya September 12 kuwa sikukuu ya Eid Elhaj.
Eid Elhaji husheherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu ambaye kufuatana na mafundisho ya vitabu vya dini alikuwa tayari ya kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Mungu. Lakini Mungu alimzuia asimchinje akampatia kondoo badala yake.