Friday, September 9, 2016
Michuano ya Olimpiki kwa walemavu yaanza huku Urusi ikinyimwa ushiriki.
Michuano ya olimpiki kwa upande wa walemavu imeanza kutimbua vumbi nchini Brazil baada ya shamrashamra za ufunguzi zilizofanyika Sept.8 kwenye uwanja wa Maracana jijini Rio de Jeneiro ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanariadha Ignas Matumla Mtweve. .
Moja ya changamoto kubwa katika michuano hiyo ni pamoja na kuwepo kwa mgogoro wa kifedha ambapo mauzo ya tiketi za ufunguzi wa michuano hiyo hayakuridhisha.
Michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu nne kutoka mataifa mia moja na sitini ulimwenguni ingawa miongoni mwa hao wanariadha wa kutoka nchini Urusi hawamo.
Wanamichezo wa Urusi wamepigwa marufuku kushiriki katika michuano hiyo kutokana na wasiwasi wa wa mattumizi ya dawa za kusisimua misuli ambazo zilipigwa marufuku michezoni,.
Comments System
facebook