Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Sunday, October 23, 2016

UKAWA wasusia uchaguzi wa Meya Kinondoni,Wagombea wa CCM wapita bila kupigwa.




Madiwani wa vyama vinavyounda umoja wa  UKAWA wamesusia uchaguzi wa Meya na naibu meya wa Halmashauri ya manisapa ya Knondoni,uliofanyika Oktoba 23,2016 hali iliyopelekea wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

Wabunge hao wa upinzani wamesusia uchaguzi huo wakinukuu sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 ambazo  haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja.

Wabunge waliolalamikiwa ni pamoja na Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga ambao waliapishwa kama madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

CCM wamemchagua Benjamini Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho ambapo George Manyanya amchagiliwa kuwa Naibu Meya.

Friday, October 14, 2016

Profesa Lipumba atupiwa virago Tanga.



WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, akikamilisha ziara katika mikoa ya Mtwara na Lindi, viongozi wa chama hicho wa Mkoa wa Tanga, hawatampa ushirikiano kama akianza ziara mkoani humo keshokutwa.

Taarifa hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama hicho, Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Jumbe alitoa msimamo huo wakati Profesa Lipumba akitarajiwa kuanza ziara hiyo ya kukiimarisha chama katika Wilaya za Muheza na Korogwe, mkoani hapa.

"Sisi hatutambui ziara hiyo na hatutashiriki kwa sababu yeye si mwenyekiti wa chama chetu kwani alishafukuzwa uanachama na baraza kuu la chama chetu"..."Kwa hiyo, narudia tena hatutashirikiana naye kwa namna yoyote ile, kwa sababu mgogoro aliouanzisha katika chama unaonyesha ni kwa jinsi gani anavyotaka kukidhoofisha chama".Alisema Jumbe.

Hata hivyo aliongeza kuwa viongozi watakaoshiriki katika mapokezi pamoja na ziara hiyo katika wilaya husika, watakuwa wamekiuka miongozo, taratibu pamoja na kununi za chama.

Chanzo:Mtanzania.

Thursday, September 15, 2016

M/Kiti UVCCM-Arusha apewa kichapo kwa tuhuma za utapeli.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mpinduzi (UVCCM) mkoani Arusha amezuiwa kuingia ofisini leo asubuhi na baadhi ya makada wa chama hicho kufuatia tuhuma zinazomkabili za kughushi nyaraka za Usalama wa Taifa na kufanyia utapeli.



Makada wa chama hicho walifunga ofisi hizo mapema leo alfajiri wakisema kuwa mwenyekiti huyo, Lengai Ole Sabaya hana hadhi tena ya kuwa mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha baada ya kughushi nyaraka za Idara ya Usalama wa Taifa kufanya utapeli.

                                   Lengai Ole Sabaya,M/Kiti UVCCM-Arusha.



Baadhi ya makada ambao ni watiifu kwa Mwenyekiti huyo wameonekana wakimsaidia aweze kuingia ofisini wakijitahidi kuwaondoa waliokuwa wakimzuia bila mafanikio.

Baadhi ya picha wakati wa vurumai hizo; 


Friday, September 2, 2016

Rais Magufuli ziarani Zanzibar,mkutano wa CUF wapigwa Stop.

      Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye majukumu yao ya ulinzi na usalama.

Chama cha wananchi CUF mapema leo kimezuiwa na jeshi la polisi kufanya mkutano wao  na waandishi wa habari ili kupisha ziara ya raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli iliyoanza mapema  leo.
 Rais Magufuli na Mkewe Mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa na wakazi visiwani humo mara baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shekhani Mohamed amedai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na eneo ambalo CUF walipanga kufanya mkutano kuwa karibu na uwanja atakaoutumia Rais Magufuli kuwahutubia wananchi.

Kwa upande wake katibu wa CUF Wilaya ya Chakechake,Salehe Nassor Juma ameelaani  na kushangazwa na maamuzi ya jeshi jeshi la polisi visiwani humo kwa madai kuwa lengo halikua kufanya mkutano wa hadhara bali mkutano na waandishi wa habari na kudai kuwa walikamilisha taratibu zote za mkutano wao ikiwemo kutoa taarifa kwenye idara ya Habari Maelezo na kupewa kibali.

Hata hivyo Katibu huyo wa CUF ameongeza kuwa dhumuni la mkutano wao lilikua ni kuunga mkono uamuzi wa baraza kuu la chama hicho kumsimamisha uanachama aliekua Mwenyekiti wa chama hicho Prf.Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wengine 10.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.