Wednesday, September 14, 2016

Neymer ageukia muziki,kuachia wimbo wiki ijayo.


Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil,Neymer ameamua kuweka wazi mapenzi yake na muziki na kwa kuthibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter alipost ujumbe kwa mashabiki wake ulimwenguni na kuahidi kuwa atatambulisha wimbo wake mpya wiki ijayo.

"This Wednesday I begin my music career and I’m going to release my first song on Facebook," Ulisomeka ujumbe huo uliotazamwa na watu zaidi ya milioni 20.

 Hii sio mara ya kwanza kwa Mwanasoka huyo kuonesha hisia zake kwenye muziki kwani March 4 mwaka 2015 ilisambaa video mtandaoni ikimuonesha yeye  na mwanasoka mwenzake Dani Alves wakiimba wimbo wa Mwanamuziki Nick Jams unaofahamika kama "El Perdon" hivyo uamuzi wa Mwanasoka huyu kuingia kwenye muziki unaonekana ni sehemu ya mipango yake ya siku nyingi

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.