Mwanamke mmoja nchini Australia anaefahamika kama Adelaide amewaita
maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka mwenye urefu wa mita 1 mwenye sumu kali
kutoka kwenye kiatu chake.
Maafisa wa Wanyama Pori Walimdhibiti Nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa akitafuta ''Joto'' ndani ya kiatu nyumbani kwa mwanamke huyo kusini mwa Australia,ambapo walimtoa ndani ya kiatu na kumtupa msituni mbali na maeneo ya makazi ya watu.
Jaimii ya Nyoka hao wenye sumu kali,hupatikana katika pwani na maeneo ya Australia.Viatu vya Mwanamke huyo aina ya buti,ni aina ya viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi ya kondoo, na hutumika sana Australia na kuvaliwa zaidi majira ya baridi kwani huwa na joto zuri.
Chanzo;BBC.