Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza timu ya taifa ya soka la wanawake ya Tanzania bara Kilimanjaro Queens kwa kutwaa kombe la baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Women’s Championship) baada ya kuifunga Kenya goli 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika mjini Jinja nchini Uganda.
Hii hapa taarifa ya Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.