Mzee,Kingunge Ngombale Mwiru ni jina kubwa kwenye siasa za Tanzania,ambapo anatajwa kama miongoni mwa waasisi wa chama tawala nchini (C.C.M),ila picha hii inayomuonesha akishuka kwenye bajaji imezua maswali mengi mitandaoni huku baadhi ya watu wakihoji kama Mzee wetu nae pesa imeadimika mfukoni mwake kama raia uraiani wanavyodai.
Ikumbukwe kuwa licha Mzee Kingunge kikutumia chama tawala (CCM) kwa zaidi miongo mitano,wakati wa uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka jana,alijivua uanachama na kujiunga na vyama vya upinzani nchini chini ya mwamvuli wa UKAWA.