Thursday, September 22, 2016
Saida Karoli ameandika haya Instagram kwenda kwa Diamond Platnumz.
Jumapili ya wikend iliyopita Diamond Platnumz aliachia wimbo mpya "Salome" akimshirikisha msanii ambae yupo chini ya lebo yake ya WCB,Ray Vany ambapo awali wimbo huu uliimbwa na Mwanamuziki wa nyimbo za asili Saida Karoli ambapo kwa wakati hit's hiyo inatoka kwa mara ya kwanza mwaka 2001 ulifahamika kama "Maria Salome".
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Saida Karoli ame-post ujumbe huu kwenda kwa Diamond Platnumz ambae uongozi wake ulifikia makubaliono ya kurudiwa kwa wimbo huo ambao ndani ya siku mbili tangu video yake ilipotoka imefikisha watazamaji milioni 1.
"Ahsante sana mdogo wngu kwa zawadi hii Mungu akujalie uzidi peperusha bendera ya nchi yetu nimefurahi sana".Ulisomeka ujumbe huo.
Comments System
facebook