Mkali wa ngoma ya Grass "Aint Greener" Chris Brown ameendelea kutokwa na mapovu siku hadi siku huku akimmwagia sifa kedekede aliyekuwa memba wa kundi la "YMCMB" mnyamwezi Lil Wayne.
Kupitia page yake ya instgram mkali huyo wa miondoko ya Pop amepost picha ikimuonyesha Lil Wayne na Yeye huku akiisindikiza na bonge la caption ambalo limeonekana kuwa ni povu lakini halikutajwa moja kwa moja limetumwa kwa nanai.
"Huyu mshikaji ana mchango mkubwa sana kwenye kazi yangu na amenipa ujasiri wa kuishi. Atabaki kuwa rappa bora kwa kipindi chote, Sio kama nyie marapa wengine msioujua hata pakuanzia, Kihalisia wengi wenu ni wanafunzi wake lakini hamtaki tu kulikubali hilo. (na ninajua kama Wayne amewaandikia nagoma nyingi sana washikaji wa Cash Money alipokua mdogo). Washikaji watataka kukushusha wakati mabo yako yakiwa mazuri lakini mwisho inabidi kudeal nao ili wapoteze kabisa ubora wao baada ya kuwapa presha.