Ulimwengu wa muziki ulitikisika mnamo June 2009 mara baada ya kifo cha Mwanamuziki maarufu na Mfalme wa Pop Michel Jackson huku kifo chake kikidaiwa kusababishwa na matumizi ya dawa za usingizi uliopitiliza ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuafnyika kwa onesho lake lilifahamika kama "This Is It" lililopangwa kufanyika jijini London.
Sasa ni miaka sita tangu MJ afariki ila mjadala wa kifo chake wiki hii ulitawala kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Marekani mara baada ya kusambaa kwa picha ya mtoto wa kike wa Mwanamuziki huyo Paris Jackson (18) ikimuonesha akiwa kwenye gari huku kwenye siti ya nyuma ikionekana taswira tata ya picha ya mtu anadaiwa kuwa na baba yake yaani Michel Jackson,picha ambayo aliifuta baada ya muda mfupi.
Kwa kudhirihirishwa kuwa Mwanamuziki huyo bado anaishi kwenye mioyo ya watu,baadhi ya mashabiki wake walichukua picha hiyo na kuitengeneza video sambamba na picha hiyo wakiamini Mfalme wa huyo wa Pop yupo hai na kuwavutia zaidi ya watazamaji 348,000.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror,mjadala mzito ulitawala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakioneshwa kuchukizwa na kitendo cha binti huyo kupost picha hiyo tata huku wengine wakihisi huenda picha hiyo ina ukweli ndani yake.
Baadhi ya Mashabiki waliandika :