Birthday Ya Aunty Ezekiel Yamshawishi Lulu, Aahidi Kuzaa Kesho
Kutoka kwenye kiwanda cha filamu za Kitanzania leo Oktoba 27 muigizaji Aunty Ezekiel anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kama ilivyo kawaida ya matumizi ya mitandao ya kijamii kila linapokuwepo tukio maalum wahusika na watu wao wa karibu hutumia mitandao hiyo kufikishiana ujumbe zikiwemo pongezi na salaam mbalimbali,
Aunty Ezekiel ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa kupost picha tofauti zikimuonyesha yeye na famil;ia yake yaani Baba mtoto wake Mose Iyobo na mtoto wa Cookie..
Elizabeth Michael "Lulu" ambae pia ni muigizaji wa Bongo muvi alishindwa kuvumilia kabisa kutokana na picha ambazo Aunty Ezekiel amezipost na kujikuta akitokwa na maneno haya ambayo wazi wazi yameonekana ni utani kwa Aunty na mtoto wake (Cookie)
"Nazaa Kesho....Nimepanic😫😫😫😫😫 @auntyezekiel najitolea kununulia album dada insta sio mahala sahihi kwa hivi vipicha vyako...tupo wanafunzi humu😭wengine bado under 18 ila naona unatushawishi😭hujui serikali inapiga vita mimba Za utotoni we dada😫Sitopenda kushawishika kwa hv vi picha vyenu 😫😫😭Cookie Ana 🐸 pia Shabaaaaaash....nadhani nimeshikwa na uchungu maana naandika caption huku nahangaika🙄😵Kesho jmn naenda kujifungua 😬😬😬😬
Sijui kama Leo ni bday yako naona kukomoa day tu😭😭😭" Ameandika Lulu..