Sunday, October 2, 2016
Brown Mauzo Kuhusu Beef Na Alikiba Na Wakenya Wanavyomchukulia
MKALI wa Muziki kutoka Kenya, Fredrick Mutinda ‘Brown Mauzo’ ameweka wazi kuwa kabla ya kutoka kimuziki Wakenya wengi walikuwa wakimuona na kumsikia tofauti na kudhani huenda ni Mtanzania.
Akipiga Stori na "Mtu Kati" ya Global TV Online Brown Mauzo pia alizima tetesi zilizokuwa zikizagaa kuwa alikuwa na bifu na Ali Kiba kisa kikiwa ni kumgomea kufanya naye kolabo.
“Hizo maneno ndiyo kwanza nazisikia huku TZ, Kiba ninavyomjua ni mtu poa sana. Uongozi wangu na wake ulikutana na kufanya naye mazungumzo ya kolabo akakubali na kusema kuwa nina kipaji kikubwa sana,” alisema Brown Mauzo.
ANGALIA VIDEO YA BROWN MAUZO NA ALIKIBA "NITULIZE"
Comments System
facebook