Sunday, October 23, 2016

PICHA:Utacheka na ujumbe wa Casper Nyovest kwenda kwa mashabiki wake kupitia maandishi aliyoandika kwenye mwili wake.


 Baada ya kushinda tuzo ya Mtumbuizaji bora wa mwaka kwenye tuzo za MTV-Mama,2016 rapper Casper Nyovest  aliwashangaza mashabiki mara baada ya ku-post video ikimuonesha akiwa kifua wazi huku mwili wake ukiwa na maandishi yaliyosomeka  "Fees must fall. See you at Orlando." akimaanisha kuwa bei za viingilio kwenye shoo yake zitashushwa.




Rapper huyo kutoka nchini Afrika kusini,anatarajiwa kufanya onesho lake kwenye uwanja wa mpira wa 'Orlando Stadium' Octoba 29 mwaka huu ambapo amedai kuwa ana uhakika wa kujaza siti 40,0000 kwenye uwanja huo na kuahidi kuwapa mashabiki wake burudani  ya masaa matatu mfululizo ambapo itakuani mara ya pili kwa Nyovest kuvunja rekodi ikiwa ni baada ya kujaza watazamaji zaidi ya 20,000 kwenye ukumbi wa Dope Arena jijini Johannesburg kwenye onesho lake lake binafsi bila kumshirikisha mwanamuziki mwingine mwezi Oktoba,2015.


Rapper huyo alitikisa kwenye mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kudai kuwa rapper kutoka nchini Marekani Kanye West aliiga aina ya uaandaaji wa jukwaa kwenye matamasha yake,hii ikiwa ni siku chache baada ya Kanye kudai kuwa kuna wanamuziki wanaiga namna anavyoandaa matamasha yake hasa uundaji wa majukwaa.

Kanye West kwenye moja ya 'tour' zake.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.