Showing posts with label Casper Nyovest. Show all posts
Showing posts with label Casper Nyovest. Show all posts
Monday, October 31, 2016
VIDEO / PICHA:Je ni kweli rapper Cassper Nyovest ameua bifu yake na AKA?,tazama alivyozaja uwanja wa Orlando Park kwenye shoo yake.
Rapper Casper Nyovest ameweka rekodi nyingine baada ya kujaza uwanja wa mpira wa miguu wa Orlando Park nchini Afrika kusini kwenye shoo yake iliyofanyika jumamosi ya tarehe 29 mwezi Oktoba 2016 hii ikiwa ni mara ya pili baada ya kukusanya watazamaji 20,000 kwenye shoo yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa 'The Dome' jijini Johannesburg mwaka uliopita.
Casper Nyovest (kulia) akikaribisha Wizkid stejini.
Uwanja wa Orlando Park ambao kwa wastani una uwezo wa kukussanya watazamaji 40,000,ulishuhudiwa ukiwa na mashabiki zaidi ya 30,000 kwenye shoo ya rapper huyo ambae alisindikizwa na wanamuziki wengine akiwemo rapper Emtee,Ricky Rick,Staa wa miondoko ya kwaito Babes Wodumo na mkali wa miondoko ya Afro-Pop Wizkid.
Ukiachilia mbali 'perfomance' kali kutoka kwa Nyovest,rapper huyo aliamsha shagwe kwa watazamaji baada ya 'live screen' zilizokua uwanjani hapo kumuonesha akikumbatiana na hasimu wake wa siku nyingi,rapper AKA ambae alihudhuria shoo hiyo akiwa kwenye eneo la wageni mashuhuri (V.I.P).
Tazama kwa ufupi sehemu ya shoo hiyo.
Sunday, October 23, 2016
PICHA:Utacheka na ujumbe wa Casper Nyovest kwenda kwa mashabiki wake kupitia maandishi aliyoandika kwenye mwili wake.
Baada ya kushinda tuzo ya Mtumbuizaji bora wa mwaka kwenye tuzo za MTV-Mama,2016 rapper Casper Nyovest aliwashangaza mashabiki mara baada ya ku-post video ikimuonesha akiwa kifua wazi huku mwili wake ukiwa na maandishi yaliyosomeka "Fees must fall. See you at Orlando." akimaanisha kuwa bei za viingilio kwenye shoo yake zitashushwa.
Rapper huyo kutoka nchini Afrika kusini,anatarajiwa kufanya onesho lake kwenye uwanja wa mpira wa 'Orlando Stadium' Octoba 29 mwaka huu ambapo amedai kuwa ana uhakika wa kujaza siti 40,0000 kwenye uwanja huo na kuahidi kuwapa mashabiki wake burudani ya masaa matatu mfululizo ambapo itakuani mara ya pili kwa Nyovest kuvunja rekodi ikiwa ni baada ya kujaza watazamaji zaidi ya 20,000 kwenye ukumbi wa Dope Arena jijini Johannesburg kwenye onesho lake lake binafsi bila kumshirikisha mwanamuziki mwingine mwezi Oktoba,2015.
Rapper huyo alitikisa kwenye mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kudai kuwa rapper kutoka nchini Marekani Kanye West aliiga aina ya uaandaaji wa jukwaa kwenye matamasha yake,hii ikiwa ni siku chache baada ya Kanye kudai kuwa kuna wanamuziki wanaiga namna anavyoandaa matamasha yake hasa uundaji wa majukwaa.
Kanye West kwenye moja ya 'tour' zake.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
facebook






