Sunday, October 23, 2016

Sauti Soul yaitoa kimasomaso A / Mashariki,huku Wizkid,Patoraking,Yemi Alade na Tekno waking'ara kwenye tuzo za MTV-Mama,2016.


Tuzo za MTV-MAMA Awards zilitolewa Octoba 22,2016 nchini Afrika kusini,ambapo kundi la Sauti Soul limewatoa kimasomaso wapenzi wa muziki na burudani Afrika mashariki baada ya kushinda tuzo ya kundi bora la muziki huku Tanzania iliyokua ikiwakilishwa na wanamuziki kama Diamond Platnumz,Vanessa Mdee,Navy Kenzo,Ali Kiba,Yamoto Band na Raymond ikitoka kapa kwenye tuzo ambazo Rapper Future kutoka nchini Marekani alitumbuiza.

Tuzo hizo ambazo awali zilipangwa kushereheshwa na Mchekeshaji Travis Noeh,zilishereheshwa na mtangazaji wa Tv nchini Afrika Kusini maarufu Bonang Matheba ambae ni X-Girl wa rapper AKA mara bada ya Travis kujitoa siku moja kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo.

Sauti Soul mbali kushinda tuzo hiyo,walikonga nyoyo za maelfu ya mashabiki kwa 'perfomance' nzuri wakishirikiana na Ali Kiba na Yemi Alade.

Wizkid aliondoka na tuzo mbili binafsi  ikiwemo ya msanii bora wa kiume na msanii bora wa mwaka huku colabo yake  na DJ Maphorisa na DJ Buckz kwenye wimbo wa 'Soweto Baby'  ikiwapa tuzo ya ya wimbo bora wa kushirikiana.

Rapper Cassepr Nyovest alikua msanii wa kwanza kutajwa kushinda tuzo,alipoondoka na tuzo ya Mtumbuizaji bora wa mwaka,kabla ya kufanya 'perfomance' fupi iliyoambatana mtindo wake mpya wa kucheza huku aki-rap.


Mwanamuziki Patoraking,alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wake wake wa 'My Woman My Every Thing' huku Yemi Alade akijinyakulia tuzo ya mwanamuziki bora wa kike.
Mwanamuziki wa mkongwe wa muziki wa Jazz nchini Afrika Kusini Hugh Masekela,alitunukiwa tuzo ya heshima ya 'Legend Awards' huku mwanamuziki maarufu wa muziki wa Kwaito, Mandoza akipewa heshima pale watazamaji walipotulia kwa dakika moja kumkumbuka Mandoza aliefariki Julai mwaka huu.

 

Artist of the Year: Wizkid (Nigeria)
Best Female: Yemi Alade (Nigeria)
Best Male: Wizkid (Nigeria)
Best Group: Sauti Sol (Kenya)
Best Breakthrough Act: Tekno (Nigeria)
Best Live Act:  Cassper Nyovest (South Africa)
Best Hip Hop in association with MTN: Emtee (South Africa)
Song of the Year in partnership with Google: “My Woman, My Everything” Patoranking feat. Wande Coal (Nigeria)
Listener’s Choice: Jah Prayzah (Zimbabwe)
Video of the Year:  “Niquer Ma Vie” - Youssoupha (Congo) - Director: Antony Abdelli & Jose Eon
Best Pop & Alternative: Shekhinah & Kyle Deutsch (South Africa)
Best Francophone: Serge Beynaud (Ivory Coast)
Best Lusophone: C4 Pedro (Angola)
Personality of the Year in association with DSTV:  Caster Semenya (South Africa)
Legend Award: Hugh Masekela
Best Collaboration in partnership with ABSOLUT: DJ Maphorisa feat. Wizkid & DJ Buckz - "Soweto Baby" (South Africa/Nigeria)
Africa Reimagined: Vivian Onano and Mary Taedzerwa
Best International: Drake (USA)





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.