Rais Magufuli na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amezuru nchini Kenya ambapo pamoja na mambo mengine amekagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21 kama ilivyo ada kwa viongozi wa mataifa wanapozurunchini humo.
Haya ni mambo matano yatakayofanywa na Rais Magufuli kwenye ziara yake nchini Kenya;
- Atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
- Atatoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
- Atahudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.
- Atatembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi
- Atazindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo jijini Nairobi.