Wakati sakata la Mshabuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza kuhusu kiwango chake na ushiriki wake kwenye timu ya taifa likiendelea kutokota,Klabu ya Manchester United imemjumuisha mtoto mkubwa wa Mshambuliaji huyo kwenye 'Academy' ya timu ya watoto ya klabu hiyo ambapo amekua akifanya mazoezi na timu ya watoto ya klabu hiyo.
Kai Wayne Rooney mwenye umri wa miaka sita ataungana na watoto wa Mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic ambae nae amewapeleka watoto wake wawili,Max (10) na Vincent (8) ambapo pia watajumika na watoto wa wakongwe wengine kama Michel Carrick,Ryn Giggs na Nick Butt ambao nao watoto wao wamejumuishwa kwenye timu hiyo ya watoto ya klabu hiyo.
Wayne Rooney na watoto wake,kwenye moja ya michezo ya Manchester United.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun,klabu hiyo imepanga kukuza vipaji vya watoto wa mastaa hao walioitumikia klabu hiyo kama sehemu ya kuenzi mchango wao na sifa waliyoipatia klabu hiyo.
"The hope at the club is some of their dad’s talent has rubbed off on the youngsters"..."Manchester United is known for its youth development, and this is just another stride towards finding stars of the future,United have some of the best youth coaches in the world, and the players know they’re in the right place".Sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.