Friday, October 7, 2016

Sababu za Rais Magufuli kitishia kumfukuza kazi mtoto wa dada yake.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametishia kumfukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANZANIA) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindikiza matunda cha Bakheresa mnamo Octoba 6,mwaka huu alipokua akifungua rasmi kiwanda cha kusindikiza matunda kilichopo Mwandege,Mkuranga mkoani Pwani kinachomilikiwa na mfanyabiashara Said Bakhresa.


Wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho kiongozi mmoja kutoka kwenye uongozi wa kiwanda hicho alipokua akielezea changamato za kiwanda hicho alisema wamekua wakikabiliwa na changamoto ya umeme na kuongeza kuwa  licha ya kuwasiliana na TANESCO tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu hali inayopelekea kutumika kwa ghrama kubwa za uendeshaji wa kiwanda hicho kutokana na kutumia jerereta kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.

 Rais Magufuli na mfanyabiashara,Said Bakhresa.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kuna kiongozi yeyote wa Tanesco mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake(jina tunalihifadhi) ambapo Rais Magufuli alimwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokua Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika kiwandani hapo kwani ni  fursa ya kibiashara.

Pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona  Tanzania inakua ya viwanda,na kama wanania kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo na kutoa miezi miwili kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho,Rais Magufuli alisema kuwa wakae na wizara ya nishati na madini na wizara ya viwanda na biashara kuona namna wanaweza kushughulikia hilo.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.