Friday, October 7, 2016

VIDEO:Bondia afariki dunia baada ya kushuka ulingoni.

Bondia Mike Towell (25),raia wa Scotland amefariki dunia baada ya kupoteza pambano lake na Bondia Dale Evans kwenye round ya tano pambano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Septemba 29,2016.

 Mike Towell,(kulia).

Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia ambapo ripoti ya Madaktari imeonesha kifo cha Mike kilisababishwa na kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara kutookana ngumi nzito alizopigwa maeneo ya kichwani.



    Mike akiwa na wapambe wake.

Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na kushindwa kuendelea na pambano.

"absolutely heartbroken".Rafiki wa karibu wa Towell,Chloe Ross aliambia mtandao wa Sky News.

 Hata hivyo Bondia Dale Evans aliepigana na Towell, ameungana na mashabiki wa bondia mwenzake hasa wa mchezo huo nchini Scotland,Wakiendesha kampeni ya kuchangisha michango kwa ajili ya familia ya Towell.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.