Sunday, October 9, 2016

Serikali ya Ethiopia yatangaza hali ya dhrarura kwa miezi sita.


Tangazo hilo limetolewa na serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu wa taifa hilo Hailemariam Desalegn baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali, yaliyofanywa na makabila mawili makubwa ya Ethiopia ya Oromo na Amhara.

Makabila hayo yanalalamika kuwa yametengwa kiuchumi na kisiasa ambapo Ghasia baina ya waandamanaji na polisi zilizidi nakupelekea watu 55 kufa katika sherehe za kitamaduni za Oromo, Jumapili iliyopita.

 Waziri Mkuu wa Ethiopia,Hailemariam Desalegn.

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema, mamia ya watu wameuawa, na maelfu kukamatwa tangu  maandamano hayo yalipoanza.
Chanzo;BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.