Saturday, October 1, 2016
Utapenda Majibu Ya Mondi Kuhusu Kiba Na MTVEMA
Diamond Platnumz amewataka mashabiki zake wampigie kura msanii Alikiba kwenye tuzo za MTV EMA akiwa kama msanii pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo.
Licha ya tofauti ambazo inasemekana wawili hao wanazo, mkali huyo amewataka mashabiki wake waweke mambo ya u-team pembeni na wajikite kwenye kuliletea taifa faida.
Akihojiwa kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow kinachoruka Cluds TV Ijumaa saa 3 usiku Diamond Platnumz alidai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Alikiba ndio maana habari za tofauti zao zinazidi kupungua siku hadi siku, na kama angekuwa na tatizo nae kweli basi ingejulikana wazi kwasababu yeye bifu lake huwa haliishi na wala sio la kujificha.
“Nimesikia Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo za MTV EMA, tufute zile zama za kusema kwasababu wewe unamsapoti Diamond ndio huwezi kumpigia kura Alikiba, kwasababu yeye akikosa tuzo hiyo haiji kabisa Tanzania na itaonekana watanzania wote tumeikosa. Kwahiyo tuhakikishe tuna VOTE ili tuirudishe tuzo hiyo nyumbani.” Alisema Diamond Platnumz.
Comments System
facebook