Showing posts with label Ali Kiba. Show all posts
Showing posts with label Ali Kiba. Show all posts

Friday, December 16, 2016

PICHA:Haya ndio mapovu ya Jokate Mwogelo kwa mmrembo huyu anaejisogeza kwa Kiba.



Kwa muda mrefu sasa Mwanamitindo Jokate Mwogelo amekua akidaiwa kuwa mapenzini  na Mwanamuziki Ali Kiba ambae hajawahi hata siku moja kukiri hadharani kutoka kimapenzi na Jokate japo wameonekana mara kadhaa kwenye matukio tofauti wakipozi kimahaba.

Huenda Jokate hafurahishwi na kitendo cha Kiba kutokiri kuwa yupo mapenzini na Jojo kiasi cha mrembo huyo kutoa mapovu yake kupitia mtandao wa Snapchat,hii ikiwa ni siku kadhaa baada ya SHILAWADU kunasa picha ya King Kiba akiwa na kimwana shombeshombe kwenye pozi flani lainii.
 Inasemekana lakini...!!















Wednesday, December 14, 2016

PICHA:ALI KIBA ALIVYOKUTANA NA YVONNE CHAKA CHAKA.




 Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambae ni Mwanamuziki bora barani Afrika mwaka 2016 kwa mujibu wa tuzo za MTV-EMA, amepost picha akiwa Mwanamama huyo mkongwe wa muziki barani Afrika na kuandika.
  
'....It was a great honor and pleasure to meet Mama Yvonne Chaka Chaka who I have loved and admired all my life . Thank you for hosting us and sharing your memories, advices and guidance. I am truly grateful and looking forward to our project #KingKiba

 Meneja wa Ali Kiba,Seven Mosha na Yvonne Chaka Chaka.

Monday, October 10, 2016

VIDEO:Baada ya kumalizika kwa Tamasha la Mombasa,Mashabiki wa Ali Kiba Kenya wamtupia lawama mitandaoni.



Baada ya kumalizika kwa tamasha la Mombasa Rocks Festival weekend hii,Tamasha lililowakutanisha mastaa wa muziki kama Chris Brown,Wizkid,Ali Kiba,Vanessa Mdee,na kundi la Sauti Soul mashabiki wa mwanamuziki Ali Kiba walioneshwa kutofurahishwa na kitendo cha hit maker wa single ya "Aje" Ali Kiba ku-perfom nyimbo chache kwa muda mfupi.

Baadhi ya post za Mashabiki wa Ali Kiba;



 Tazama Ali Kiba alivyo-perfom kwenye Tamasha hilo; 

Monday, October 3, 2016

Tegemea Kumsikia Ali Kiba Kwenye Koilabo Na Navy kenzo


Baada ya KAMATI CHINI pamoja na nyimbo ya GAME kupenya katika mipaka ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kundi matata la muziki kutoka TANZANIA linaloundwa na couples wawili AIKA pamoja na producer bora wa mwaka 2015-2016 NAHREEL wameingia jikoni na kupika hits nyingine kibao ikiwemo colabo ambayo tayari imefanywa pamoja na ali kiba


 Lakini pia Navy kenzo limekuwa kundi pekee ambalo limechaguliwa kutoka TANZANIA kupeperusha bendera  kwenye msimu mpya wa nne wa COKESTUDIO AFRIKA ambayo inafanyikia nchini kenya


Vile vile kundi hilo limekuwa nominated katika tuzo mbili  kubwa AFRIKA MTV MAMA zitazofanyika october 22 SOUTH AFRICA ukumbi wa ticket pro Dome pamoja na wats up tv africa video music award 2016 za GHANA




Hivyo wanawaomba mashabiki wao kuwa pigia kura  kama kundi bora kutoka Afrika ili wapate kunyakua tuzo hiyo





Saturday, October 1, 2016

Utapenda Majibu Ya Mondi Kuhusu Kiba Na MTVEMA

 http://thedouglasreview.com/wp-content/uploads/2016/04/Diamond-Platnumz.png
 Diamond Platnumz amewataka mashabiki zake wampigie kura msanii Alikiba kwenye tuzo za MTV EMA akiwa kama msanii pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo.
Licha ya tofauti ambazo inasemekana wawili hao wanazo, mkali huyo amewataka mashabiki wake waweke mambo ya u-team pembeni na wajikite kwenye kuliletea taifa faida.
Akihojiwa kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow kinachoruka Cluds TV Ijumaa saa 3 usiku Diamond Platnumz alidai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Alikiba ndio maana habari za tofauti zao zinazidi kupungua siku hadi siku, na kama angekuwa na tatizo nae kweli basi ingejulikana wazi kwasababu yeye bifu lake huwa haliishi na wala sio la kujificha.
“Nimesikia Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo za MTV EMA, tufute zile zama za kusema kwasababu wewe unamsapoti Diamond ndio huwezi kumpigia kura Alikiba, kwasababu yeye akikosa tuzo hiyo haiji kabisa Tanzania na itaonekana watanzania wote tumeikosa. Kwahiyo tuhakikishe tuna VOTE ili tuirudishe tuzo hiyo nyumbani.” Alisema Diamond Platnumz.

Sunday, September 18, 2016

Picha:Msichana aliejichora tatoo ya Ali Kiba baada ya kupagawishwa kitandani.

Wakati Ali kiba na Diamond walipokutana kwenye jukwaa moja mjini Mombasa kuna mambo mengi yaliyotokea nyuma ya pazia.Miongoni mwa issue zilizo-trend baada ya show kumalizika ni pale ambapo mrembo mmoja anaefahamika kama Bridget Achieng  alipoamua kuvujisha siri nzito kati yake na Ali kiba baada ya kuamua kuchora mchoro wa tatoo wenye jina la hit maker wa singo ya "Aje",Ali Kiba.
 Tetesi  zinadai kuwa,mrembo huyo alifikia uamuzi wa kuchora tattoo hiyo ya "King Kiba" baada kupagawishwa na shughuli ya Kiba kitandani kiasi cha kuamua kuchora tattoo hiyo kama  sehemu ya kukubali mtiti wa sita kwa sita kutoka kwa Mwanamuziki huyo.

A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him
Mrembo huyo amedai kuwa alijisikia mtu mwenye bahati kwa kuwa msichana pekee aliepata nafasi ya kumliwaza msanii huyo wakati alipokua mjini Mombasa na kuongeza kuwa tatoo hiyo itabaku kama kumbukumbu kwenye maisha yake kuwa aliwahi ku-kwichi-kwichi na King Kiba.
 A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him


A besotted Kenyan girl gets a tattoo of Ali Kiba, says she'd die for him

Image result for ali kiba




Tuesday, September 13, 2016

Music | Barakah The Prince Ft. Alikiba - Nisamehe Mp3

BarakadaPrince amekutana na King Kiba kwenye mdundo wa Emmatheboy wakatengeneza kitu kinaitwa nisamehe,
 Fanya kuidownload hapa chini halafu tuambie maoni yako kuhusu ujio wa ngoma hii.





Baraka Da Prince na Naj wafundishana Kingereza huku wanakula Denda:

Thursday, September 8, 2016

Diamond,Ali Kiba na Ya Moto Band watajwa kuwania tuzo za Afrima.

Tuzo za Afrima zinazoandaliwa kwa ufadhili wa taasisi ya African Union Commission (AUC)     zimetangazwa huku orodha kamili ya wasanii wanaowania tuzo ikimjumuisha Msanii wa Bongo Fleva,
Diamond anaewania vipengele vitano.

Viepengele hivyo ni pamoja na  Songwriter of The Year in Africa, Song of The Year in Africa, Artiste of The Year, Best Artist in Africa na Best Male Artist in Eastern Africa.

Watanzania wengine waliotajwa kwenye tuzo hizo ni pamoja na Alikiba anayewania cha Best Male Artist in Eastern Africa na Yamoto Band likitajwa kuwania kipengele cha Revelation of The Year.
Tazama orodha kamili,


 afrima



afrima1

afrima2

afrima4
afrima5afrima4afrima6afrima3


afrima8
 afrima9

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.