Monday, October 31, 2016

VIDEO / PICHA:Je ni kweli rapper Cassper Nyovest ameua bifu yake na AKA?,tazama alivyozaja uwanja wa Orlando Park kwenye shoo yake.


Rapper Casper Nyovest ameweka rekodi nyingine baada ya kujaza uwanja wa mpira wa miguu wa Orlando Park nchini Afrika kusini kwenye shoo yake iliyofanyika jumamosi ya tarehe 29 mwezi Oktoba 2016 hii ikiwa ni mara ya pili baada ya kukusanya watazamaji 20,000 kwenye shoo yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa 'The Dome' jijini Johannesburg mwaka uliopita.

 Casper Nyovest (kulia) akikaribisha Wizkid stejini.


Uwanja wa Orlando Park ambao kwa wastani una uwezo wa kukussanya watazamaji 40,000,ulishuhudiwa ukiwa na mashabiki zaidi ya 30,000 kwenye shoo ya rapper huyo ambae alisindikizwa na wanamuziki wengine akiwemo rapper Emtee,Ricky Rick,Staa wa miondoko ya kwaito Babes Wodumo na mkali wa miondoko ya Afro-Pop Wizkid.



Ukiachilia mbali 'perfomance' kali kutoka kwa Nyovest,rapper huyo aliamsha shagwe kwa watazamaji baada ya 'live screen' zilizokua uwanjani hapo kumuonesha akikumbatiana na hasimu wake wa siku nyingi,rapper AKA ambae alihudhuria shoo hiyo akiwa kwenye eneo la wageni mashuhuri (V.I.P).


Tazama kwa ufupi sehemu ya shoo hiyo.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.