Vitabu vya dini vinasema, mwanamke atazaa kwa uchungu. Lakini
wanawake wa siku hizi hawataki na wanaogopa kuzaa kwa uchungu hali iliyopelekea Madaktari kufanya utafiti na kutafuta dawa na njia mbalimbali kuhakikisha kuwa Mama mjazito anajifungua kwa raha
mustarehe.
Wapo wanawake wengine ambao wanadiriki kuwaomba madaktari wawazalishe
kwa kisu mara tu mtoto anapotimia ili mradi kukwepa maumivu ya uchungu
ambayo mama hukumbana nayo wakati wa kujifungua.
Wakati wanawake wakiamua kuzaa kwa njia ya upasuaji ili kukwepa
maumivu ya mtoto kutoka tumboni, wanasayansi nao wamegundua njia mbadala
ya kumfanya mwanamke asihisi uchungu wakati wa kujifungua hii ikiwa ni baada ya utafiti kuonesha kuwa nyoka mwenye sumu kali zaidi duniani huenda akawa jibu la kupatikana kwa dawa ya kupunguza uchungu.
Nyoka anayeitwa ‘Blue Coral’ ndiye mwenye sumu kali zaidi na
hupatikana zaidi Kusini Mashariki mwa Bara la Asia. Utafiti mpya
uliochapishwa kwenye jarida la afya la 'Toxin' umesema nyoka huyo
huwalenga maadui wake wakiwemo nyoka wenzake,ambao husababisha uchungu kwa binadamu.
Wanasayansi kupiatia utafiti wao wakiongozwa na Dkt.Brian Fry research of Dr. Brian Fry wanasema huenda sumu hii ikatumika kutengeneza dawa ya
uchungu. Baadhi ya wanyama ambao sumu yao imetumika kutengeneza dawa za aina hii ni
pamoja na Konokono wa baharini na Bui bui wa sumu.
Wanasayansi sasa wanataka nyoka huyu kuhifadhiwa hususani baada ya
maeneo mengi anakopatikana kugeuzwa kuwa mashamba ya michikichi.
Wanasayansi walifanya utafiti wao katika nchi za China, Singapore na
Marekani ambapo hao wanadai kuwa japo kwa mwanadamu nyoka huwa adui, lakini wakati huu huenda akawa suluhu la matatizo mengi ya kiafya.