Monday, November 7, 2016
Wanandoto Ya Kalla Jeremiah Yaibua Maajabu Ya Kweli..
Mwanamuziki Kalla Jeremiah amesema video ya wimbo wake "Wanandoto" umewakutanisha mama na mtoto wake waliopoteana kwa zaidi ya mwaka mmoja.
kama unavyoweza kuona hapo kwenye picha ni mtoto Adam ambae alipotezana na mama yake na picha ya chini ni Adam alipokutana na mama yake mzazi baada ya kupoteana kwa muda mrefu.
"MAAJABU YA KWELI .
KAMA SIKU TATU ZILIZOPITA NILIPOKEA SIMU KUTOKA KWA MTANGAZAJI WA RADIO FLANI AKANIELEZA KUWA KUNA MAMA ALIMPIGIA SIMU AKAMWAMBIA KUWA AMEMUONA MTOTO WAKE ALIYEPOTEA TOKEA MWAKA JANA MWEZI WA 9 NA KAMUONA KWENYE VIDEO YANGU YA #WANANDOTO KIUKWELI NILISHTUKA NIKAOMBA MTANGAZAJI YULE ANIUNGANISHE NA MAMA HUYO. NIKAFANIKIWA KUONGEA NA MAMA HUYO NA KWELI AKANIAMBIA ALIPOTELEWA NA MTOTO WAKE AITWAE ADAM NA KWAMBA KAMUONA MWANAE KWENYE VIDEO YANGU. YULE MAMA AKASEMA AMEHANGAIKA SANA KUMTAFUTA MWANAE KWA UTARATIBU WA KAWAIDA HADI KWA WAGANGA MBALIMBALI WA KIENYEJI BILA MAFANIKIO AKASEMA PIA AMEENDA KWENYE MAOMBI MBALIMBALI LAKINI HAKUWEZA KUMPATA MTOTO WAKE NA AKAKATA TAMAA KABISA.HALI HIYO YA KUMPOTEZA MTOTO WAKE IMEMUATHIRI SANA KIASI CHA KUWA ANAZIMIA MARA KWA MARA. BAADA YA MAELEZO YALE NIKAMUUNGANISHA MAMA HUYO NA MLEZI WA KITUO CHA WATOTO CHA CHAKUWAMA NA JANA AMEFANIKIWA KUFIKA KITUONI HAPO NA KUMUONA MWANAE KWA KWELI HUU NI MUUJIZA.
ADAM NDO HUYO ALIYEZUNGUSHIWA KIDUARA CHEUSI NA PICHA YA CHINI NI ADAM AKIWA NA MAMA YAKE MZAZI JANA" ameandika Kalla Jeremiah kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Comments System
facebook