Sunday, December 11, 2016

J.Cole anavyovunja rekodi zake mwenyewe kupitia album zake bila 'Colabo' na Mwanamuziki yeyote.


Rapper J. Cole huenda akavunja rekodi ya mauzo ya  album ya 'Platnum' bila kumshirikisha mwanamuziki yeyote kwa mara ya pili kupitia album yake mpya inayofahamika kama '4 YOUR EYES ONLY' kama alivyofanya awali na album yake ya '2014-FOREST HILL DRIVE'.

Kwa mujibu wa  HITS Daily Double, album hiyo  mpya yenye jumla ya nyimbo 10 inatabiriwa kufikisha mauzo ya nakala 550,000 hadi 575,000 kwenye wiki yake ya kwanza tangu  ilipoingia sokoni ikiifutia album ya rapper Drake inayofahamika kama 'VIWES' ILIYOUZA  jumla ya nakala milioni 1.4 na 'LEMONADE' ya Mwanamuziki BeyoncĂ©  iliyouza nakala 653,000 kwenye wiki yake ya kwanza.

Takwimu hizi zinamfanya J.Cole kuwa na wiki ya kihistoria kwenye maisha yake ya kimuziki,hii ikiwa ni baada ya album yake ya '2014-FOREST HILL DRIVE' iliyotoka mwaka 2016 kuvunja  rekodi ya mauzo ya 'Platnum' mara mbili kwa maana ya kuuza nakala milioni 2 na kufika hadi namba 1 kwenye chati za  Billboard 200 ikiwa imeuza jumla ya nakala 371,000.


Album hiyo mpya ya Cole ambayo kabla ya kutoka kwake ilitanguliwa na 'Documentary' aliyoipa jina 'EYES',kwa sasa inashikilia namba 1 kwenye kwenye mauzo ya album kwenye mtandao wa iTune huku singo tatu kutoka kwenye album hiyo,ikiwemo 'Deja Vu',Immortal' na 'Neighbors' zikiwemo kwenye Chati ya nyimbo 20 bora za mtandao huo.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.