Baada ya kurudi uraiani ikiwa ni wiki moja tangu alipolazwa hospitali kutokana na maradhi ya msongo wa mawazo,rappper Kanye West amerudi kwenye vichwa vya habari baada ya kukutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Kikao baina ya wawili hao kilichofanyika kwenye jengo la Trump Tower,New York City kilitajarajiwa kufanyika hii ikiwa ni baada ya rapper huyo kudai kuwa ingawa hakupiga kura anaamini kura yake ingeenda kwa Trump alieibuka mshindi dhidi ya Hillary Clinton.
"I don’t mean that I don’t think that Black Lives Matter,I
don’t mean that I don’t think I believe in women’s rights...because that
was the guy I would’ve voted for".Kanye West aliwaambia mashabiki waliohudhuria shoo ya tour yake ya 'Sant Pablo Tour',ambapo hata hivyo aliamua kuikatiza shoo hiyo baada ya kuporomosha dhidi ya vyombo vya habari,watu maarufu akiwemo swahiba wake wa siku nyingi Jay Z.
Ingawa haijawekwa wazi juu kilichojiri kwenye kikao chao,ila Rais Trump kwa kifupi ameeleza kuwa yeye na Kanye ni marafiki wa siku nyingi ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter West amedai amesogeza mbele mipango yake ya kugombea urais wa Marekani hadi 2024 ili kumpa Trump nafasi ya kumsafisihia njia.