Tuesday, December 13, 2016
VIDEO/KUTOKA IKULU:Rais Magufuli aongoza kikao cha halmashauri kuu ya CCM.
Wakati akifungua mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 355 Rais Magufuli ameondoa utata wa kikao hicho cha Chama hicho tawala kufanyika Ikulu na kudai kuwa vyama vingine vinavyotaka kufanya mikutano yao Ikulu vinaweza kuomba ila watahitaji kujua ajenda zao na kuongeza kuwa haoni aibu ya kuwakaribisha wana CCM Ikulu maana asingefika hapo na kudai kuwa Ikulu mahali pa watanzania wote.
Aidha Rais Magufuli ameelezea mipango ya serikali yake kununua Meli mbili moja ziwa ya ziwaTanganyika na nyingine ya ziwa Victoria na kuongeza kuwa anahitaji kuona chama hicho kikijitegemeea kiuchumi kwani ni ni aibu kwa chama kutegemea fedha za ruzuku na watu binafsi ili kujiendesha.
Chanzo:Azam Two Tv.
Comments System
facebook