Baba Platinum a.k.a Abdul Juma (hapo anafikiria Chapaa) |
Ukitaja Top Ten ya Artist ambao ngoma zao zinafanya poa kwenye vituo mbalimbali ya radio bongo, huwezi kuacha kulitaja jina lake, ukitaja Top ten ya Celebs ambao habari zao zina mek head line katika section Tabloid bongo basi huwezi kukosa kulitaja jina la Nasib Abdul /Diamond Platinum, kwa zaidi ya wiki moja hivi na ushee kulikua na habari kuwa kuna mzee amejitokeza na kudai kuwa yeye ni baba mzazi wa msanii huyo, na akatoa lawama nyingi kwa Diamond kwa kutokuwa na mawasiliano mazuri na yeye tangu apate mafaniko ya kimuziki, sasa akijibu mapigo Diamond amesema "Nisingependa kuskia baba anavyosema simjali na naendekeza starehe, si kauli nzuri kwa sababu ina maana amenijua mimi mwanae sasa hivi baada ya kujua nimekua Diamond? Siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenilea na kunisomesha mpaka kuwa hivi, lakini aliniacha nikalelewa na mama yangu kwa shida na tabu zote mpaka leo nikawa hivi, so nisingependa kuskia mtu anazungumzia yeye ni mzazi wangu kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana wakati wa maslahi" akaongeza kwa kuusifia uwezo wa akili yake "Nilipokua mdogo nilikua naitwa Koffi Olomide(msanii wa congo msomi) kwa sababu nilikua nina akili za darasani na nilikua napenda kuimba pia".