Sunday, February 16, 2014

NYOKA AKATISHA MAISHA YA PASTOR KANISANI

Pastor Jamie Coots akiwa kwenye moja kati ya Ibada
Mtumishi wa mungu Jamie Coots aliyekua anaamini Katika wokovu wa kutumia Nyoka amefariki dunia katika mji wa Kentucky nchini marekani baada ya Nyoka aliyekua anaabudu nae kanisani kumng'ata, inasemekana gari la Kubeba wagonjwa lilifika hadi nyumbani kwake kwa ajili ya kutoa msaada, Pastor huyo wa kanisa la kipentekoste akawafukuza wahudumu hao wa hospitali na baada ya Saa moja kupita Pastor akafariki dunia,
Inadaiwa kwa mujibu wa  kanisa la "Snake Salvation wanaamini biblia inasema waking'atwa na Nyoka basi sumu yake haiwezi kuwadhuru kwasababu wapo na nguvu ya mungu,  Kanisa hilo limekuepo kwa miaka karibu mia, na Pator Jamie Coots amerithi imani hii kutoka kwa babu yake, na amekua akitoa neno kwa kutumia Nyoka tangu mwaka 1994



Hii sio mara ya kwanza kwa Pastor huyo kutendwa na nyoka, amewahi kukatika kidole baada ya kung'atwa na Nyoka na jeraha lile aliliacha mpaka kidole kikaoza 
Kidole cha Pastor kilichokatika kwa jeraha la Nyoka
Angalia video ya moja kati ya Ibada za Nyoka zilizowahi kuongozwa na Pastor Jamie Coots

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.