Showing posts with label U Heard. Show all posts
Showing posts with label U Heard. Show all posts

Friday, October 21, 2016

U - HEARD | Msanii Wa Bongoflava Afumaniwa Akipenzika Na Mke Wa Mtu

Mjini siku hizi kuna wadudu wafekenyuzi wa mambo wanaitwa Shilawadu hata ufanye jambo la siri ukiwa peke yako watajua tu...
 Leo shilawadu wamemfikishia Mhariri mkuu wa Gazeti La Makorokocho Ubuyu tena video kabisa ya mwanamuziki wa Bongoflava akishushiwa kichapo mara baada ya kufamaniwa akipenzika na mke wa mtu...
Picha linaanza mwenye mke wake alisafiri ndugu yete akahamia kwa baby kubebika maraia si wakamtonya mwenye mke akiwa safarini akatuma majeshi yake..
Unataka kuupata Ubuyu Mzima?  Bonyeza Play Kwenye Video Hii Hapa Chini

Wednesday, May 7, 2014

YOU HEARD: NASH MC AKATAA KUZUNGUMZIA TUHUMA ZA KUMTUNDIKA BINTI MIMBA NA KUIKATAA


Rapper Nash Mc amekataa kuzungumzia Tuhuma zilizotolewa na Mwanadada Subira dhidi yake, awali mwanadada huyo alidai kuwa zaidi ya miezi mitano iliyopita alikua katika mahusiano na Msanii huyo na akatundikwa mimba lakini alipojaribu kumwelezea mpenzi wake ambaye ni Nash Mc eti alipinga kuhusika na Ujauzito, sasa nilipocheki na Nash Mc akajibu yeye hawezi kuzungumzia ishu hizo kwani yeye sio doctor na anachoweza kuzungumzia ni CD yake anayotaka kuitoa hivi karibuni, nilipoendelea kumuuliza kama anamfahamu Subira Nash aliijibu "HipHop" HipHop HipHop

Friday, March 14, 2014

YOU HEARD - WEMA APIGWA NA DIAMOND KISA VICTORIA KIMANI

Jana Usiku wakati Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz pamoja na mwanadada Victoria Kimani walikua wana record ngoma katika Studios za T.H.T wakati wakiwa wana Record ghafla akatokea mchumba wa Diamond na kuanza kulalama kuwa bwana wake yuko katika mapenzi na Victoria Kimani, inasemekana wawili walipishana Lugha hatimaye wakaanza kupigana hali iliyosababisha Wema kushindwa na kutokomea zake ili kuepusha shari zaidi.

Wednesday, March 5, 2014

YOU HEARD : HATIMAYE SHILOLE NA NUH MZIWANDA WAFUNGISHWA NDOA, Hihihihihihiiii

Shilole
Hatimaye Penzi la shilole na Msanii mwenzake Nuh Mziwanda lipo waziwazi baada ya Mziwanda kufunguka kwenye Mic ya Gossip Cop, kuanzia walivyoanzisha mahusiano yao mpaka mipango yao ya baadae.

Maongezi kuhusu mahusiano yao yalianza baada ya mimi kuwaona wakiwa Pamoja kwenye Uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro Dar Live Mbagala, nikamuuliza Shilole Vipi tena mbona usiku usiku na Nuh, Shilole akanijibu ni rafiki yangu ni msanii mwenzangu, ndipo Nuh alipoingilia maongezi kwa kusema "Anakudanganya huyo, muongoo" Shishi Mpenzi wangu, mke wangu mtarajiwa, muda si mrefu ntakuletea mwaliko wa ndoa, nategemea kumuoa, tumeanzisha mahusiano kama miezi miwili au mitatu iliyopita, nashkuru mungu tunapenda kweli, hakuna mambo ya Umarioo, nilikaa muda mrefu bila Girlfriend,

Shilole na Nuh Mziwanda ndani ya Club Masai Jumamosi iliyopita

Tuesday, March 4, 2014

YOU HEARD : SHILOLE AONYESHA NGUO YAKE YA NDANI JUKWAANI

Mwanadada Shilole wakati akiwa ana perform katika Uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro iliyoandaliwa na Zamaradi Mketema, jumamosi iliyopita Shilole alijikuta akisaula na Kuwaonyesha mashabiki wake nguo ya Ndani hali iliyowafanya mijibaba iliyokua na uchu itoe mimacho sambamba na Udenda kuwadondoka kwa mbaali, huku wakishangilia kutoa ishara arudi tena na tena, sasa aliposhuka jukwaani nikamkamata na kumtupia maswali, Shilole alionyesha ushirikiano na hata nilipomtania kwa kumwomba anionyeshe na mimi hakusita na kunionyesha na kuniambia mbona ni kawaida, nahisi kidogo alikua amechangamka kwa Alcohol kidogo au sijui ndo maamuzi yake sijui, ila mwenyewe anasema anamzimia sana Mwanamama Tshela Mwana kutoka Congo msanii ambaye ni maarufu kwa kusaula anapokua Jukwaani,

Usiku huo Shilole alikua ameambatana na Wacheza show wake pamoja na msanii wa Kiume 'Nuh Mziwanda' ambae inasemekana wako katika dimbwi zito la mahaba, nikamuuliza vipi mbona usiku usiku na Nuh? akanijibu ni rafiki ni msanii mwenzake, ndipo Nuh alipoibuka na kuniambia 'Muongo huyooo, sio kweli kwamba mimi ni rafiki yake au msanii mwenzake, sisi ni zaidi ya Hivyo' sasa ukitaka kujua maongezi kati yangu na Shilole pamoja na Nuh Mziwanda, usikose Kuskiza XXL Kesho Pyaaaaaaaaaaaaaa.....
Nuh Mziwanda

Wednesday, February 12, 2014

U HEARD : SHILOLE KATI KATI YA PENZI LA MADEE NA NUH MZIWANDA (INASEMEKANA LAKINI)



Inasemekana Eti Msanii wa Bongo Flava ambaye pia ni Muigizaji wa Bongo Movie Mwanadada Shilole kwa wakati huu yuko katika mahaba mazito na Up Coming Artist Nuh Mziwanda lakini kabla ya kuwa na Nuh Eti alikua anatoka na msanii mkongwe wa Bongo Flava Madee,

Madee
Sasa utata umeibuka baada ya Shilole Kuandaa Show Kijijini Kwao Igunga Tabora akawa ameamua kuwachukua Nuh na Madee pamoja  Queen Darlin waende kushambulia Jukwaa la Igunga, hadi matangazo yalikua yameshatengenezwa lakini kumbe Madee alikua Hajui kama katika Show Hiyo Nuh ataenda, taarifa zilizofika mezani kwa muhariri zinadai kuwa eti Madee aliposhtukia mchongo kuwa Nuh pia anaenda, ikabidi amshtue meneja wake ambaye ni Babu Tale awaambie kina Shilole kuwa kama Nuh Mziwanda ataperform katika Show hiyo basi yeye Madee haendi Igunga,

Nuh Mziwanda
Ujumbe ulipomfikia Shilole akapima uzito wa wasanii hao mwisho wa siku akaona poa Bora Nuh abaki Dar kwa sababu hana nguvu ya kuvuta mashabiki wakati Madee ana uhakika akiwepo basi watu kibao watajitokeza, Show ya Shilole Mkoani Tabora inatarajiwa kufanyika Weekend hii inayokuja ya Valentine, inasemekana Lakini

Tuesday, February 11, 2014

U HEARD : UKWELI KUHUSU PENZI LA DIVA NA GK

Diva
 Hivi karibuni taarifa zilisambaa kwenye mtandao kwamba kuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya Mastar wawili Diva (Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho) na King Crazy GK Legendary wa Muziki wa Bongo Flava, Jumatatu iliyopita Muhariri nilipiga Story na GK akafunguka kuwa nimcheki Diva, yeye hakuwa na jibu, sasa siku ya Jumanne nikacheki na Diva na hivi ndivyo alivyofunguka


Monday, February 10, 2014

U HEARD: CRAZY GK NA DIVA KATIKA DIMBWI ZITO LA MAHABA INASEMEKANA LAKINI

Crazy Gk
Tetesi ambazo zipo kitaa inasemekana kwamba Bongo Flava HipHop Legendary Crazy GK yuko katika mahaba mazito na Mtangazaji wa Kipindi cha Ala Za Roho ya Clouds fm Mwanadada Loveness Love a.k.a Diva, Historia inasema Diva amewahi kuwa katika mahusiano na Bongo Flava Artist Mo Racka, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe, na Rapper CMB Prezzo wa Kenya Inasemekana Lakini, pia Crazy Gk inasemekana amewahi kuwa katika mahaba mazito na msanii Nakaaya Sumari pamoja na Jackline Cliff, Na sasa hivi ndo hivyo Mastar hawa wawili wameamua kunonihino a.k.a Kwichy Kwichy Skiza Segment ya You Heard kama ilivyokua leo kwenye XXL ya Clouds fm

Wednesday, July 24, 2013

U HEARD : JAMAA AMWAGA CHOZI BAADA YA KUMFUMANIA WIFE WAKE NA DIRECTOR WA BONGO MOVIE (ENOCK KOBELO)


KATIKATI NI ENOCK KOBELO MUONGOZAJI WA FILAMU WA SAUTI NA PICHA
Jamaa mmoja anayeishi maeneo ya Ubungo, Juzi kuamkia jana majira ya saa 5 usiku alimfumania wife akiwa na mdau wa Bongo Movie anayefahamika kwa jina la Enock Kobelo (Director & Editor) kabla ya kuwafumania Emanuel amefunguka kuwa siku ya Tukio yeye alimkuta wife wake anaongea na simu, akamuuliza anaongea na nani? akajibiwa kuwa "Naongea na Kaka Yangu" jamaa akatilia shaka simu hiyo, basi wakati wakiwa wamekaa za ndani mara message ikaingia kwenye simu ya Wife wake, Jamaa akampokonya simu mke wake na kutoka nayo Nje, kuichungulia akashtukia kuwa ni ujumbe uliotumwa na Mwanaume ambaye walikuwa wanapanga na huyo mwanadada wakutane kesho yake ili wakafanya mambo ya chumbani, basi jamaa akaendeleza ile chat huku akijifanya yeye ndo yule mwanamke na kumwambia bwana Enock Kobelo njoo usiku huu, Kobelo midadi ikampanda vuuup akaibuka mpaka ubungo akidhani kuwa alikua ana chat na yule mke wa mtu, kufika akazama mpaka chumbani kwa wale wanandoa, Mwenye Mke alikua nje anaangalia chezo loooote, basi baada ya muda akafata nyuma lakini mlango akakuta umefungwa kwa ndani ndo ikabidi avunje na kuzama ndani, lahaulaaaaaaaaaaaa
anakuta Wife wake yuko na Upande mmoja wa Kanga ndembendembeeee, Jamaa Huyo (Emanuel) huku akiwa ameshika Panga, Kisu Na Bisibisi akamuamrisha Kobelo avue Suruali alipoona anabisha bishaa akamlazimisha na kuanza kukata ule mkanda mpaka nguo boxer zikashuka, Timbwili ndo lilianzia hapo ile anataka kugusisha Ndude yake kwenye makalio ya mgoni wake ndo akatokea polisi mmoja anayeishi chumba cha jirani na kumnasua Emanuel ili asije kuzamisha Ndude yake kwa mchizi, Polisi alipofanikiwa kesi ikahamia katika Kituo cha polisi jirani.
Skiza sauti hapo chini upate mchapo mzima.

Skiza na Muendelezo


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.