Weusi kampuni yenye members kama lord eyez, joh makini, bonta, Nikki wa
pili na g nako wameazimia kujenga maktaba 100 katika vijiji 100 kwa
kushirikiana na watanzania,
msemaji wa weusi Nikki wa Pili
amefunguka kwamba kila mtanzania atachangia shillingi 100 kwa ajili ya
kutengeneza maktaba 100 katika vijiji 100 na kila maktaba iwe na vitabu
100, na uchangiaji huo utakua kwa njia ya simu za mkononi, na wamebakiza vitu kidogo kuanzisha harambee hii.
Weusi kesho watakua ndani ya Escape 1 kupiga show ya "Funga Mwaka la Weusi"