Usiku wa kuamkia leo Diamond platnumz ameamsha popo tena kwa kuitetea
africa mbele ya priyanka chopra star mkubwa india na dunia nzima kwa ujumla
ambaye ametajwa mara kadhaa kuwa ni mwanadada mrembo kuliko wote barani asia,
ilikua ni kwenye utoaji wa tuzo za mtv ema ambapo mwaka huu tukio lilifanyika italy, na diamond platnumz amefanikiwa kuchukua tuzo ya best worldwide act africa/india
Diamond ameandika maneno mazito kwenye page yake ya instagram kwamba "Hii sio tunzo yangu ni tunzo ya wewe na mimi maana bila kura yako nisingeweza kabisa kushinda... naomba niwashkuru sana sana kwa kura zenu Mashabiki zangu pendwa... wasanii wenzangu, Media, Uongozi pamoja na familia... bahati mbaya Kutokana na harakati za uchaguzi hatuta weza kuwa na mapokezi ila ukipita tutaandaa siku maalum kwa wote tuweze piga picha nayo"
Diamond amechukua tuzo hii ambayo tangu mtv ema waanze
kuiita Best worldwide Act tangu mwaka 2011 tuzo hiyo imechukuliwa mara
tatu na wasanii wa morocco
Abdel fatah grini na ahmed sultan, na mwaka jana ilichukuliwa na
msanii raia wa palestina
Kupata tuzo yoyote ya mtv ema ni ndoto kwa kila
msanii wa africa, ukiangalia vizuri list ya wasanii wakubwa wanaofanya muziki
wa kizazi kipya wa africa ni wachache sana wamewahi kupata tuzo lakini wengi
wameishia kwenye nomination
Davido pia hajawahi kupata tuzo hizi ila
mwaka jana alikua nominated tu.
2013 wizkid aliishia kuonja nomination
tu.
D banj aliwahi kuikwarua tuzo ya best
african act mwaka 2007
2face pia amewahi kukwarua tuzo ya best
african act
Pongezi sana kwa Diamond Platnumz.