Kupitia Instagram ndugu yetu Idris Sultan amefanya kile kilichotafsriwa kama kisasi kwa shemela wetu Wema Sepetu ambae siku ya jumatatu alipost picha ya mastaa tofauti huku akiwataja kama #MCM's wake (Yaani Wanaume Wanaomvutia) akiwemo zilipendwa wake "Diamond Platnumz" aka Bba Tiffah. kama unavyoona hapa chini.
Sasa jana jumatano Idris nae akaitumia siku hiyo kumpost yule aliyemtaja kama #WCW wake huku akisindikiza na hashtag yake #TusichukulianePoa.
Idris alipost picha tatu za mrembo huyo huku akiahidi kutopost tena kwenye mtandao kwa siku ya jana.
Mapichapicha hayakuishia hapo
Idris aliendelea kumnadi #WCW wake huku akiendelea kuipa nguvu hashtag yake #TusichukulianePoa
Idris alimaliza kwa post hiyo na muda mfupi baadae ikasemekana Idris Sultan amefuta akaunti yake ya Instagram, Snitch wetu hakutaka kukubali ikabidi aende kwenye page ya Idris ili kujiaminisha alichosikia na haya ndiyo majibu aliyokutana nayo.
ANGALIA HAPA VIDEO MPYA YA SAMATA A- KODO