Wikiendi iliyopita Mwimbaji wa hitsong "Jike Shupa" Nuh Mziwanda amenusurika kuchezea kichapo baada ya mashabiki kuanzisha vurugu zilizopelekea Nuh Mziwanda kushuindwa kuendelea na show iliyofanyika pande za Mtwara.
Nuh Mziwanda amesema alishindwa kuendelea na show baada ya kuimba jike shupa na mashabiki wake kutaka aendelee na wimbo huo huku wengine wakitaka aimbe nyimbo zake nyingine.
Baada ya mvutano kuwa mkubwa Nuh aliamua kuondoka lakini alikanusha ishu ya kupigwa kama ubuyu wa awali ulivyonyetisha.
Ubuyu mwingine uliopo mjini ni kuhusu picha ya Nuh Mziwanda na malkia wa vichupa Amber Lulu
Inasemekana Nuh Mziwanda ameamua kufanya hivyo kufuatia mapicha picha yanayoendelea mtandaoni yakimuonyesha mpenzi wake wa zamani yaani Shilole akiwa na mpenzi wake mpya.
Akijibu Swali aliloulizwa na Soudy Brown wa You Heard ya Clouds FM , Nuh Mziwanda alikanusha kwa kusema hamjui Amber Lulu na akimuona atamchana kufuatia usambaaji wa picha hiyo kwani Kiki hazitafutwi kwa style hiyo.
Kuhusu Shilole na mpenzi wake mpya Nuh Mziwanda amesema ni kitu cha kawaida sana na anaona kila kitu kiko sawa.