Wednesday, September 21, 2016

Picha: "Kenya Here We Come",Trey Song atua Kenya.

 Hit maker wa ngoma kali za R&B kutoka nchini Marekani,Trey Song yupo nchini Kenya tayari kwa msimu mpya wa Coke Studio.


Kupitia mtandao wa Snapchart usiku wa kuamkia leo,Trey Song aliwathibitishia mashabiki wake ulimwenguni kushiriki kwenye msimu mpya wa Coke Studio kwa ku-post   "Slow Motion Video"  iliyoambatana na maneno "Kenya Here We Come".
Mshindi huyo wa tuzo za Grammy na kipenzi cha warembo,atakua akirekodi nyimbo katika msimu mpya wa Coke Studio na ku-perfom live na mastaa wengine wa muziki kutoka Afrika kama,Nyanshisk(Kenya),Vanessa Mdee(Tanzania),Stonebwoy(Ghana),Neyma(Mozambique),Yemi Alade(Nigeria) na Emtee(SouthAfrica).

 Trey Song akishiriki chakula na Yemi Alade.

 Trey Song akiwa ndani  ya usafiri wa umma maarufu kama "Matatu" kwenye mitaa ya Jiji la Nairobi.


 

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.