Zuckerberg akiwa na mastaa nchini Nigeria.
Alienda nchini humo kwa kushtukiza Jumanne hii na kutembelea kituo cha masuala ya teknolojia huko Yaba mjini Lagos. Kulikuwa na ulinzi mkali na wengi kwenye kituo hicho kiitwacho CcHUB, hawakujua kama atawatembelea.
"Ni mara yangu ya kwanza kuja Afrika chini ya jangwa la Sahara. Nitakutana na watengenezaji na wajasiriamali na kujifunza kuhusu mwenendo wa makampuni machanga,” taarifa hiyo iliandikwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.Licha ya kutembelea kituo hicho cha mafunzo ya teknologia Zuckerberg alitembea kwenye mitaa ya jiji la Lagos bila ulinzi wa kutosha ambapo pia alionekana akifanya mazoezi kwenye daraja la Lekki Bridge nchini humo.
Ugali samaki vepeee....!!