Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa samani ambazo ni mali za Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe katika jengo la Club Bilicanas,katikati ya Jiji la Dar es salam,jengo ambalo pia ni Ofisi za Free Media (Tazania Daima) kutokana na mmiliki huyo kudaiwa
malimbikizo ya kodi takribani bilioni moja.
Kiongozi huyo wa kambi ya upinzani nchini alipewa notisi na shirika hilo iliyofikia mwisho wake mwezi Otober mwaka huu ambapo alitakiwa kulipa malimbikizo ya kodi.