Sunday, September 11, 2016
Tetemeko la ardhi latokea tena mkoani Kagera.
Taarifa za awali kutoka mkoani Kagera zinaeleza kuwa tetemeko la ardhi jingine limeukumba mkoa huo ikiwa ni saa chache baada ya kugwa kwa watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko lililotokea Septemba 10.
Baadhi ya mashuuda wamedai kuwa tetemeko hilo sio kubwa kama lililotokea jana na kupelekea maafa makubwa na pia leo limedumu kwa sekunde chache zaidi.
Watu wamesikika wakipiga kelele katika harakati za kutoka kwenye makazi yao ili kunusuru uhai wao.
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu ili kukupatia taarifa rasmi.
Comments System
facebook