Wednesday, September 21, 2016

Utafiti waonesha glasi moja ya bia humfanya mtu kutaka kujuana na watu zaidi.



Watafiti kutoka Uswisi wamethibitisha  kuwa glasi moja ya bia humfanya mtu apate uwezo wa kutaka kujuana na watu zaidi  kiasi cha kuweza kutoa dukuduku lake la moyoni.

Kundi la watafiti kutoka hospitali ya Chuo Kikuu cha Basel wamewafanyia utafiti watu 60 ambapo nusu kati yao walipewa bia na wengine wakapewa kinyaji kingine tofauti kabisa na bia na watu hao wakashiriki kwenye matukio tofauti tofauti.

Profesa Matthias Liechti ambae alikua Matafiti mkuu amesema watu wanaokunywa bia kwa wstani ni wachangamfu na walionekana kuwa na shahuku na kujuana vyema na watu wengi kuliko wale ambao hawakunywa bia.Pia amethibitisha kuwa wanaokunywa  bia hushirikiana kwa pamoja katika masuala mengi ya kimaisha,kubadilishana mawazo ila akasisitiza kuwa unywaji wenyewe usiwe wa kupindukia.

Mapema mwaka huu serikali ya Uingereza ilitoa masharti mapya ya unywaji wa pombe.ambapo ushauri wa serikali ulipendekeza wananchi wasinywe bia zaidi ya glasi saba ambapo hatua hii ilifikiwa baada ya ushahidi kuonesha kuwa unywaji wa pombe kupindukia unamuweka mtu katika hatari ya kuugua saratani ya matiti.

Hata hivyo tafiti tofauti kuhusu unywaji wa bia zinadai kuwa ili mradi mtu anakunywa kwa wastani basi atakua na furaha na pia inazuia kujihusisha na ngono kiholela.

Sasa mdau wetu tuambie....kwa uzoefu wako,unafikiri utafiti huu una ukweli ndani yake...?

#Shilawadu.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.