Thursday, October 6, 2016

Diamond amtetea Mama yake kwa kuto-post picha ya Zari.


Katika mahojiano aliyofanya kituo cha redio cha Times Fm,Diamond Platnumz aliulizwa kwanini mama yake hakuweka mtandaoni picha ya Zari wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa lakini aliweka picha ya Wema Sepetu alipokua akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa na kama ni kweli kuwa kuna ugomvi kati Mama yake na Zari,Diamond alisema haya.

"Sisi ndio pambo la mitandao,Mtu akiamka lazima aingie kwenye familia ya kina Diamond ajue inafanya nini,ni familia ambayo ina mashikamano na ipo kibiashara zaidi".

"Inabidi tuwape watu vitu vya kuzungumza zaidi,Kila kinachofanyika kinafanyika kwa makusudi na Mama yangu na Zari wanaelewana sana,ndio maana Zari yupo Tanzania kwa sasa".

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.