Monday, October 10, 2016

Drake avunja rekodi ya Michel Jackson kwenye tuzo za American Music Awards 2016.


Wanaowania tuzo za American Music Awards 2016 wametangazwa ila cha kushangaza kwenye tuzo hizo mwaka huu rapper Drake ameongoza kwa kutajwa kwenye vipengele 13 kwenye tuzo hizo,akivunja rekodi ya King of Pop Michel Jackson alietajwa kuwania vipengele 11 mwaka 1984 kwa mujibu wa kituo cha ABC.

 Colabo ya wimbo alioshirikishwa na Rihanna "Work" imeongoza kwa kutajwa kwenye vipengele saba huku Wanamuziki Adele na Justin Bieber wakitajwa kwenye vipengele vitano kila mmoja.Hata hivyo Mwanamuziki Beyonce's na The Chainsmokers wametajwa kwenye vipengele vinne kila mmoja.

Hata hivyo mastaa hao watakabiliwa na upinzani kwa Wanamuziki wengine wanaowania tuzo hizo kama
Selena Gomez, Ariana Grande, Twenty One Pilots, Carrie Underwood, na Mwanamuziki The Weeknd falietajwa kwenye kipengele cha  “Artist of the Year.”

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.