Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM.
Taarifa
kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana
nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na kumtupa baadaye
bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas Mashali walimuokota na kumpeleka
hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.